Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri leo amefungua mafunzo ya saratani ya malngo wa kizazi katika Ukumbi Mkubwa wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa. Mafunzo hayo ni ya siku moja na yametolewa na wataalam toka Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa wakiongozwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Said Mawji ambao walipatiwa mafunzo toka Wzara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime, Wakuu wa idara wa Halmashuri ya Wilaya ya Mpwapwa, wakuu wa taasisi, wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, maafisa tarafa na viongozi wa dini toka Wilaya ya Mpwapwa.
Katika hotuba yake Mkuu wa Wilaya amesema " Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wa chanjo wametuambia itaazisha chanjo mpya ya kuwakinga na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 kuanzia mwezi April, 2018 nchi nzima. Serikali imeamua kuanza kutoa chanjo hii kwasababu saratani ya mlango wa kizazi ndiyo inayoongoza kwa kuua wanawake wengi ukilinganisha na saratani nyingine hapa Tanzania."
Mhe. Jabir Shekimweri (Katikati) Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Saratani ya Mlango wa kizazi wilayani Mpwapwa (Picha Na: Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA, Mpwapwa)
Pia ametaja visababishi vichache vya saratani hiyo ni pamoja na kuanza kujamiana katika umri mdogo,kuwa na wapenzi wengi,kuwa na ndoa za matala,kuzaa watoto wengi, na vutaji wa sigara. Vilevile Mhe. Kimweri ameorodhesha baadhi ya dalili za salatani ya mlango wa kizazi kama vile kutokwa damu ya hedhi bila mpangilio, kutokwa damu baada ya kujamiiana,maumivu ya mgongo, miguu na/au kiuno, kuchoka, kupungua uzito, kupungukiwa au kokosa hamu ya kula,kutokwa uchafu wa rangi ya kahawia au wenye
damu kwenye uke,maumivu ya miguu au kuvimba. Dalili mbaya zaidi zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kuishiwa damu, figo kushindwa kufanya kazi, kupatwa na fistula, na uvimbe wa tezi.
Mhe. George Fuime (aliyesimama) Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa akiipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa kujali afya za wananchi wake na kugharimia chanjo hii. Mhe. Fuime amesema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya chanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi wilayani Mpwapwa (Picha Na: Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA, Mpwapwa)
Pia amewaomba wadau wote walihudhuria mafunzo haya wasaidie kupeleka ujumbe huu wa kuanzishwa kwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa mabinti wa miaka 14 ili waweze kukingwa na madhara makubwa yanayoweza kuwapata hapo baadae ya kuugua kwa maumivu makali sana na hatimaye kifo. Wengi wetu tumetembelea Ocean Road na kuona
jinsi jamaa zetu wanavyopata mateso makali.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa umakini mafunzo ya saratani ya mlango wa kizazi Wilaya ya Mpwapwa (Picha Na: Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA, Mpwapwa)
Mwisho amewataka wanchi wote kujitokeze kwa wingi katika kuzungumzia chanjo hiyo katika hali chanya na kuwaondoa wananchi wote wasiwasi kuwa chanyo ni salama na haina madhara.
Dkt. Said Mawji (aliyesimama), Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa akitoa mafunzo ya saratani ya mlango wa kizazi na kuelezea chanjo ya saratani hiyo.
Kwa habari zaidi pakua nyaraka hizi hapa chini:
HOTUBA-MKUU WA WILAYA YA MPWAPWA JUU YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI.pdf
MIKAKATI WA KIMKOA KUHUSU UZINDUZI WA CHANJO [Compatibility Mode].pdf
Saratani ya mlango wa kizazi.pdf
HALI HALISI YA UPIMAJI MLANGO WA KIZAZI [Compatibility Mode].pdf
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.