.
1.0 UTANGULIZI
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ilipanga kukusanya na kutumia jumla ya shilingi 11,521,931,774.00 katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2016/2017 sawa na asilimia 32 ya bajeti nzima ya Halmashauri ya Wilaya inayofikia shilingi bilioni 36,504, 001,974.00 baada ya kupungua kwa ukomo wa bajeti, Kiasi hiki ni nje ya bakaa ya shilingi 2,154,293,906.02 zilizobaki ilipofika tarehe 30 Juni 2016. Mchanganuo wa fedha hizo za maendeleo na vyanzo vyake ni kama unavyoonekana katika jedwali:-
NA |
CHANZO |
KIASI |
% |
1 |
Halmashauri (Own Source)
|
1,885,691,410.00 |
16 |
2 |
Ruzuku Serikali Kuu
|
9,636,240,364.00 |
84 |
|
JUMLA
|
11,521,931,774.00 |
100 |
2.0 MAPATO
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imepokea kiasi cha shilingi 5,798,883,870.12 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo sawa na asilimia 50.3 ya makisio ya shilingi 11,521,931,774 zilizotengwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017, hadi ilipofika tarehe 31 Machi , 2017. Maeneo yaliyopokea fedha ni Barabara, CDG, BUSKET FUND, Mfuko wa Jimbo, Mfuko wa elimu Equip na Mfuko wa jamii (TASAF).
3.0 MATUMIZI.
Hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2017 kiasi cha shilingi 4,369,786,821.03 kimetumika kati ya shilingi 7,953,177,776.14 zilizokuwepo (ikiwa ni salio hadi tarehe 30 Juni, 2016 ya shilingi 2,154,293,906.02 na fedha pokelewa kipindi cha Julai – Machi kwa mwaka 2016/2017 shilingi 5,798,883,870.12). Matumizi haya ni sawa na asilimia 54.9 ya fedha zilizopokelewa zimeendelea kugharamia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa katika Wilaya kwenye sekta za Elimu, Kilimo na mifugo, Afya, Maji na Barabara.
4.0 UTEKELEZAJI;
Utekelezaji wa miradi unaendelea kwa kutumia Fedha zilizovuka mwaka na zilizopokelewa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017, hivyo miradi mingi inayoendelea kutekelezwa ni ya viporo kwa mwaka 2015/2016.
Ili Kuweza kupata Orodha ya Miradi na Hali ya Utekelezaji wake Bofya hapa : MIRADI ROBO III 2017.pdf
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.