Huduma za Afya
Wilaya ina Hospitali moja (1), Vituo vya Afya vinne (4), zahanati 52 kati ya hizo za Serikali ni 48, mashirika 3 na binafsi moja (1). Vijiji 46 kati ya vijiji 113 vilivyopo Wilayani vina vituo vya huduma ya afya sawa na asilimia 40.7 ya mahitaji yote.
Jedwali Na.1; Idadi ya vituo vya kutolea huduma
Na
|
Aina
|
Mahitaji
|
Zilizopo
|
Pungufu
|
% ya upungufu
|
1
|
Hospital
|
1
|
1
|
0
|
0
|
2
|
Vituo vya Afya
|
33
|
4
|
29
|
87.9
|
3
|
Zahanati
|
113
|
52
|
61
|
53.9
|
Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa ina jumla ya vijiji 113 na ili kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na Zahanati na kila kata inakuwa na kituo cha afya, Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa inaendelea kutenga fedha katika bajeti yake kila mwaka pia kushirikisha nguvu za wananchi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya, majengo ya Zahanati pamoja na nyumba za watumishi katika maeneo mbalimbali. Kwasasa tunaendelea na ujenzi wa Zahanati tisa (9) , Majengo ya kutolea huduma (OPD) vituo vya afya vine (4) na Nyumba za watumishi mbili (2).
Magonjwa ya Mlipuko
Idara ya afya kupitia timu ya wataalamu wake kuanzia tarehe 16 Februari 2016, walienda kufuatilia taarifa za wagonjwa wa kuharisha na kutapika katika wilaya, sambamba na ugawaji wa dawa na vifaa tiba vya kupambana na kuzuia kuharisha na kutapika katika zahanati za kutolea huduma. Hata hivyo wagonjwa watatu waliripotiwa kufariki hadi tarehe 16 Machi 2016
Chanjo
Katika kukabiliana na tatizo la vifo vya akina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga na walio chini ya miaka mitano, mkakati uliopo ni kuhakikisha kwamba akina mama wote wenye uwezo wa kuzaa pamoja na watoto chini ya miaka mitano wanapata chanjo ili kujikinga na magonjwa yanayozuilika. Hali ya uchanjaji inaridhisha kwa kuwa kwa watoto chini ya miaka mitano uchanjaji ni zaidi ya asilimia 80 na kwa akinamama wajawazito ni zaidi ya asilimia 90
Jitihada zilizopo katika kukabiliana na vifo vya akina mama na watoto
Kuendelea kuelimisha Jamii juu ya afya ya uzazi na uzazi salama kwa kushirikisha wanaume
Kuendelea kuelimisha wakunga wa jadi kuwasindikiza wajawazito katika vituo vya kutolea huduma na kuendelea kutoa motisha wa fedha kwa wakunga wa jadi kwa kutumia fomu maalum inayotumika kumpa rufaa mjamazito kutoka kwa mkunga wa jadi ili kwenda kwenye vituo vya afya.
Kuendelea kuhamasisha mama wajawazito wenye vidokezo vya hatari kwenda kwenye nyumba ya kusubiria kujifungua yaani Chigonela.
Programu za afya - Mfuko wa Afya ya Jamii
Jumla ya kaya 15,984 kati ya 66,316 tayari zimejiunga na mfuko. Mapato yanayotokana na Mfuko huu yametumika kuboresha huduma zitolewazo katika vituo vya huduma kama vile ununuzi wa vitendea kazi, madawa, ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya vituo husika.
Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa
Wanachama wameendelea kuongezeka kadri watumishi wapya wanavyoajiriwa na vilevile huduma zimekuwa zikitolewa na kuboreshwa hata pale Hospitali au vituo vya afya vinapokuwa havina dawa wanachama wanapewa fomu maalumu kwenda kupata dawa au vifaa tiba katika maduka ya dawa muhimu ya watu binafsi.
Programu za UKIMWI
Utekelezaji wake ni wa kuridhisha japo kumekumbwa na tatizo la vitendea kazi. Aidha kumekuwa na changamoto ya kutokuwepo kwa wakati kwa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV). Huduma hii inatolewa katika vituo 5.
Katika kuendeleza vita dhidi ya UKIMWI, elimu na semina zinatolewa kwa vijana, wazee na makundi maalum. Serikali ya Marekani kupitia Shirika lisilo la kiserikali la TUNAJALI imejenga majengo ya Kliniki za matibabu na uangalizi wa wagonjwa wa UKIMWI katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Programu za Kifua Kikuu
Matibabu na upimaji wa wagonjwa unaendelea pamoja na ushirikishwaji wa mradi wa UKIMWI kwa wagonjwa wenye magonjwa yote mawili. Huduma inatolewa katika vituo 5.
Vifaa vya kuhudumia wagonjwa
Serikali imekuwa ikitoa vifaa kwa ajili kutolea huduma mbalimbali katika vituo vya huduma kulingana na aina na ngazi ya kituo. Hivi sasa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ina CD4 machine 1, X-ray machine 1, Ultra-sound machine 1, Biochemical machine 1, Kiti maalumu kwa ajili ya kutolea matibabu ya meno pamoja na vifaa vinginevyo vya tiba na uchunguzi,hata hifyo bado mahitaji ya vifaa ni makubwa
Upatikanaji wa madawa
Serikali kupitia Mpango wake wa ILS (Intergrated Logistic System) imekuwa ikitoa madawa pamoja na vifaa tiba katika vituo vyote vya kutolea huduma vya Serikali kulingana na mahitaji ya kituo husika na hivyo kuvifanya vituo vya huduma kuwa na dawa pamoja na vifaa vya kutosha.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.