USURI WA IDARA
UTANGULIZI:
Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana ni miongoni mwa Idara na Vitengo 19 vinavyouunda Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Idara ina jukumu la kuwasaidia wananchi binafsi au katika makundi kuelewa uwezo wao katika kutambua changamoto au mahitaji yao ya kimaendeleo au uwezo wao katika matumizi ya fursa na raslimali zinazopatikana katika maeneo yao katika kutatua changamoto hizo za kimaendeleo ili kujipatia kipato na kujiletea maendeleo na kuimarisha kiwango cha maisha kwa njia ya kujitegemea na msaada kutoka Serikalini na kwa wadau wa maendeleo.
MATARAJIO/NIA YA IDARA
Kuwawezesha wananchi kuelewa uwezo wao katika kuainisha changamoto, kuchambua na kutafuta utatuzi wa changamoto hizo kwa kutumia uwezo walionao na raslimali zinazopatikana katika maeneo
kuwawezesha wananchi wenye raslimali (ardhi, mifugo n.k) zitumike kubadilisha mfumo wao wa maisha kimaendeleo
Kuwahimiza wananchi kuanzisha vikundi vya kiuchumi vya wanawake, vijana, watu wenye ulemavu, na makundi mengine kwa madhumuni ya kupambana na umasikini
Kuimarisha kanuni za utawala wa bora katika Halmashauri za Vijiji
kuelimisha jamii kuondokana mila, desturi na imani zinazokwamisha au zuia maendeleo
Kuongeza uelewa wa jamii na wananchi walio wengi juu ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI
MUUNDO WA IDARA
Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana imegawanyika katiak Vitengo vitatu (3), sehemu nne (4) na inasimamia programu nne (4) kama ifuatavyo:
A.VITENGO NA SEHEMU
1.0 Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
1.1 Jinsia na Maendeleo
1.2 Maendeleo ya Vijana
1.3 Uratibu wa Asasi Zisizo za Kiserikali (AZAKI)
1.4 Ufundi, Ujenzi na Teknolojia
2.0 Kitengo cha Ustawi wa Jamii
3.0 Kitengo cha Maendeleo ya Vijana
B. PROGRAMU ZA IDARA
1.0 Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
2.0 Udhibiti UKIMWI
3.0 Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
4.0 Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (Dawati)
HALI YA WATUMISHI
Ili idara iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo kulingana na miundo ya Utumishi iliyopo inatakiwa kuwa na watumishi wapatao 209, waliopo kwa mwaka 2016/17 ni 18 na upungufu ni 191 kwa mchanganuo ufuatao:
NA
|
KADA/CHEO
|
MAHITAJI
|
WALIOPO
|
UPUNGUFU
|
1
|
Mkuu wa Idara
|
1 |
1 |
0 |
2
|
Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Vijiji
|
113 |
0 |
113 |
3
|
Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Kata
|
33 |
4 |
29 |
4
|
Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Wilaya (desk officers)
|
10 |
10 |
0 |
5
|
Maafisa Ustawi wa Jamii ngazi ya Wilaya (desk officers)
|
13 |
2 |
11 |
6
|
Maafisa Ustawi wa Jamii Wasaidizi Kata
|
33 |
0 |
33 |
7
|
Maafisa Maendeleo ya Vijana
|
2 |
0 |
2 |
8
|
Mafundi Sanifu
|
4 |
1 |
3 |
|
JUMLA
|
209
|
18
|
191
|
MALENGO, WAJIBU NA MAJUKUMU YA IDARA
Malengo ya Idara
Idara ina malengo makuu ainishi matatu ya Kuboresha huduma na kupunguza maambukizi ya VVU/ UKIMWI, Utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na vitendo vya Rushwa pamoja na kuboresha Ustawi wa Jamii, Jinsia, na kuwezesha jamii katika Maendeleo
Wajibu na Majukumu makuu ya Idara
Kuhamasisha na kuwezesha jamii kupanga na kutekeleza shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo
Kusaidia utayarishaji wa mipango ya jamii/wananchi kwa kutumia mbinu mpya ya Jitihada za Jamii yenyewe (Community Initiatives)
Kuwezesha jamii kuunda vikundi vya ujasiria mali, kiuchumi na kijamii
Kuhamasisha jamii juu ya masuala ya jinsia na maendeleo
Kuunganisha wadau mbalimbali katika shughuli za maendeleo
Kuhamasisha jamii katika kukabiliana na maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI
Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa shughuli mbalimbali chini ya Programu za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Udhibiti UKIMWI, Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Kuandaa na kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa vikundi, jamii juu ya ujasiriamali, utawala bora na Haki za binaadamu
SERA MBALIMBALI ZA IDARA
Katika utekelezaji wa wajibu na majukumu ya Idara inazingatia Sera zifuatazo za Kisekta:
A: Sera ya Maendeleo ya Jamii ya 1996
Lengo kuu la sera hii ni kuiwezesha jamii, watu binafsi,familia, vikundi, Asasi za Kiraia (AZAKI) na wadau wengine kuchangia zaidi kwenye nia na juhudi za Serikali ya kuinua ari kujitegemea na kuleta maendeleo katika ngazi zote
B: Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya 1996
Lengo kuu la Sera hii ni kuhakikisha kuwa kila Mtoto anapata haki zake za msingi zikiwemo:
C: Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya 2000
Lengo kuu la Sera hii ni kuanzisha mazingira mazuri kwa wanawake na wanaume kutimiza wajibu wao katika jamii na kuondoa tofauti za ushiriki wa wanawake katika masuala ya maendeleo kwa kujenga uwezo wao katika maamuzi na kutenda
D: Sera ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya 2001
Lengo kuu la Sera hii ni kuanzisha mazingira mazuri yatawezesha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuendeleza na kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa jamii.
E: Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003
Madhumuni ya jumla ya sera ni kuhakikisha kuwa wazee wa Tanzania wanatambuliwa na kupewa fursa ya kushiriki katika mambo yanayohusu maisha ya kila siku kwa manufaa ya Watanzania wote. Aidha kuhakikisha kwamba wazee wanapata huduma zote muhimu na za msingi ambazo zitawawezesha kushiriki kwa ukamilifu katika maisha ya kila siku ya Watanzania
F: Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya 2007
Malengo ya jumla ya Sera hii ni kuwasaidia, kuwawezesha na kuwaongoza vijana na wadau wengine katika utekelezaji wa masuala ya maendeleo ya vijana
G: Sera ya Taifa ya Watu Wenye Ulemavu ya Mwaka 2004
Lengo la Sera hii ni kuimarisha hali ya maisha ya watu wenye ulemavu kwa kuwapa moyo (encourage) katika maendeleo ya watu wenye ulemavu, kuwezesha familia zao, kufanya mapitio au marekebisho ya sheria ambazo sio rafiki kwa watu wenye ulemavu, kuimarisha huduma zao, kuruhusu watu wenye ulemavu kushiriki kwenye maamuzi na kushiriki utekelezaji wa shughuli muhimu katika jamii na kuruhusu familia za watu wenye ulemavu na jamii kwa jumla kushiriki katika maamuzi ya shughuli rafiki kwa watu wenye ulemavu.
H: Sera ya Taifa ya Uwezeshaji wananchi Kiuchumi ya 2004
Lengo la msingi la Sera hii ni kutoa mwongozo wa jumla utakaohakikisha watanzania walio wengi wanafikiwa na fursa na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi katika sekta zote za uchumi
I: Sera ya Taifa ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI ya 2001
Lengo la jumla la Sera hii ni kuweka mfumo wa uongozi na uratibu wa kitaifa wa mwitikio kwa virusi vya UKIMWI na ugonjwa wa UKIMWI
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.