UTANGULIZI.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ni mojawapo ya Halmashari zilizoundwa kwa Mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya mwaka 1982 sura ya 287 kama ilivyohuishwa mwaka 2002.
Halmashauri imeundwa na idara pamoja na vitengo ambapo kitengo kimoja wapo ni Kitengo cha sheria.
KAZI ZA KITENGO
Pamoja na majukumu mengine Kitengo cha Sheria jukumu lake la msingi ni kutoa ushauri wa kisheria kwa Halmashauri na Wananchi kwa ujumla.
Kitengo hutoa ushauri na maelekezo mbalimbali kwa mabaraza ya Kata pale kilipotakiwa kufanya hivyo.
Kesi na Mashauri Mbalimbali
ZIFUATAZO NI KESI AMBAZO ZIKO MAHAKAMANI NA AMBAZO ZIMETOLEWA MAAMUZI
S/NA.
|
JINA LA KESI NA NAMBA.
|
MADAI HALISI
|
HATUA
|
MAAMUZI
|
HALI HALISI
|
1.
|
Khamis Shaban Malongo Vs Halmashuri ya Wilaya Mpwapwa
Madai ya Ardhi no.110/2010 Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya Dodoma. |
Mdai alifungua madai kuwa Halmashauri imejenga shule ya Sekondari Mwanakianga katika eneo linalobishaniwa bila ridhaa yake.
|
Halmashuri ilishindwa na kutakiwa kumlipa mdai Tshs 40,016,600/= ikiwa ni fidia na gharama za kesi.
|
Baraza liliamuru akaunti ya Halmashauri ikamatwe ili kufidia deni hilo ambapo Halmashauri iliweka pingamizi na kufungua mapitio ya mwenendo wa kesi na amri za kukamata akaunti husika ambayo ilifutwa mnamo tarehe 29/10/2015 kwa kukosa uwakilishi .
|
Kesi imepangwa kutajwa tarehe 13/02/2017
|
2.
|
TALGWU vs Halmashauri ya Wilaya ya mpwapwa NA Halmashauri nyingine 11 other council
Madai na. 555/2015 Mahakama kuu Dar es Salaam. |
Wadai walifungua kesi wakidai kufukuzwa kazi kinyume na taratibu.
|
Katika mahakama ya Kazi Dar Es Salaam wadai walishindwa kesi na kukata rufaa Mahakam kuu Dar es Salaam ambayo pia ilifukuzwa kwa kufunguliwa nje ya mda.
|
Wadai wamefungua maombi ya kupeleka rufaa nje ya muda ambapo halmashauri ziliweka pingamizi.
|
Kesi imeondolewa mahakamani kwa kukiuka masharti ya sheria wadai wameruhusisiwa kufungua upya kesi hiyo baada ya kurekebisha kasoro hizo za kisheria.
|
3.
|
ADOSTA INVESTMENT CO.LTD VS MPWAPWA DISTRICT COUNCIL
Kesi Na.4/2016 |
Mdai alifungua kesi katika Mahakama kuu ya Dodoma akidai Halmshauri kuwa ilivunja Mkataba dhidi yake bila kufuata taratibu na anadai fidia ya jumla ya Tsh. 433,000, 000/=.
|
Halmashauri ya Wilaya ilipeleka majibu mahakamani ambapo katika majibu iliweka madai dhidi ya Kampuni hiyo (Counter Claim).
|
Kesi ya msingi imetupiliwa mbali kwa gharama baada ya pingamizi la awali la kisheria kutolewa maamuzi.
|
Kesi ilitolewa maamuzi tarehe 08/12/2016na Halmashuri ilishinda kesi hiyo.
|
4.
|
ERASTO YOHANA MLEWA VS BEREGE VILLAGE COUNCIL.
Kesi No. 5/2016 |
Mdai alifungua kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa dhidi ya Serikali ya Kijiji cha Berege kutaka mahakama iamuru alipwe fidia baada ya kushinda katika kesi ya jinai No.85/2012 iliyohusu uhalifu wa mabomba ya maji na kuwa alipwe fidia kwa madhara aliyoyapata ya jumla ya Tsh. 36,388,000/=.
|
Halmashauri ya Wilaya ilipeleka majibu mahakamani ambapo katika majibu iliweka mapingamizi ya kisheria (PO) kwa mdai kutofuata taratibu za kisheria.
|
Mapingamizi yamekubaliwa.
|
Maamuzi yalitolewa tarehe 04/10/2016 na Serikali ya kijiji imeshinda kesi hiyo.
|
5.
|
MAKUTUPA VILLAGE VS JOBU CHALO
Maombi Na. 184 /2016 |
Halmashauri ya Kijiji cha makutupa ilifungua maomba dhidi ya Mlalamikiwa katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya baada ya Mlalamikiwa kuvamia eneo la kijiji na kuliomba baraza litoe tamko kuwa eneo linalobishaniwa ni mali ya Serikali ya Kijiji na Kijiji kilipwe gharama za kesi.
|
Halmashauri iliomba zuio (stop order) kumzuia mlalamikiwa kuendelea kuvamia eneo hilo.
|
Baraza lilikubali maombi hayo na kuweka zuio kuendelea kuvamia na kutumia eneo lenye mgogoro.
|
Kesi ilitolewa hukumu tarehe 17/11/2016 ambapo Baraza lilisema kesi hiyo ilishasikilizwa na kutolewa maamuzi na Baraza la kata na Mahakama ya Wilaya, kijiji kimefungua mapitio (Revision) katika Mahakama kuu Dodoma na imepangwa kutajwa tarehe 13/02/2017
|
6.
|
FRANKO SIPRIAN KIBURUNGE VS CHOGOLA VILLAGE
|
Mrufani alishitakiwa na Serikali ya Kijiji cha Chogola kwa kuvamia ardhi ya kijiji katika Baraza la Kata ambapo Serikali ya Kijiji ilishinda kesi hiyo. Baada ya kutoridhika na maamuzi hayo alipeleka rufaa katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya Dodoma.
|
Majibu ya sababu za rufaa yalipelekwa Barazani.
|
Kesi hiyo inasikilizwa kwa njia ya maandishi (Written Submissins)
|
Kesi ilitolewa maamuzi tarehe 07/12/2016 ambapo kijiji kilishinda rufaa hiyo.
|
7.
|
STARCOM CONSUMER HEALTH CARE LTD VERSUS MPWAPWA DISTRICT COUNCIL
|
Mdai alifungua kesi katika Mahakama kuu ya Wilaya Mpwapwa mnamo tarehe29/11/2017 akidai Halmshauri pesa ambazo haijamlipa kwa huduma aliyotoa ya chakula katika Hospitali ya wilaya ambapo anadai jumla ya Tsh. 50,784, 400/=, riba ya 25% na fidia.
|
Majibu yalipelekwa Mahakamani.
|
Kesi haijaanza kusikilizwa
|
Kutajwa tarehe15/02/2017
|
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.