Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni mojawapo kati ya vitengo vilivyo chini ya Idara ya Utawala katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Kitengo hiki kinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Dira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ya kuwa Taasisi inayomjali mteja katika utoaji wa huduma kwa ajili ya maendeleo endelevu ifikapo 2025. Pia inatekeleza Mwelekeo wa halmashauri ya Mpwapwa wa kuwapatia wananchi wake huduma bora za kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia misingi ya utawala bora. Hivyo basi Lengo kuu la kitengo hiki ni kuhakikisha miundombinu ya TEHAMA katika Halmashauri inakuwa bora na salama katika utoaji wa huduma.
Majukumu ya Kitengo cha TEHAMA
Majukumu ya kitengo cha TEHAMA ni kama ifuatavyo;
Malengo ya Kitengo kwa Mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/2017
Malengo kwa mwaka wa fedha 2015/2016
Kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Kitengo kilijiwekea malengo yafuatayo;
Malengo kwa mwaka wa fedha 2016/2017
Watumishi na Vitendea kazi.
Watumishi
Jedwali hapo chini linaonesha mahitaji na hali halisi ya watumishi katika Kitengo cha TEHAMA kwa sasa.
Na
|
Kada |
Mahitaji |
Waliopo |
Mapungufu |
1
|
Mchambuzi wa mifumo ya Kompyuta (System Analyst II)
|
2 |
2 |
0 |
2
|
Fundi sanifu wa Kompyuta (Computer Technician)
|
1 |
0 |
1 |
|
Jumla
|
3 |
2 |
1 |
Pamoja na upungufu wa Mtumishi huyo uliopo, kitengo kimeweza kutekeleza majukumu yake. Pia kama kungekuwa na vitendea kazi vya kutosha kitengo cha TEHAMA kingeweza kutekeleza majukumu yote ipasavyo (matengenezo ya vifaa vya TEHAMA, kusimami na kufunga LAN).
Vitendea Kazi
Pamoja na upungufu wa vitendea kazi, kitengo kinavyo vitendea kazi kama ilivyoorodheshwa katika jedwali hapo chini;
Vifaa vya ofisi
Na |
Kifaa |
Idadi |
Hali |
Maelezo |
1. |
Crimping tool
|
2 |
Nzima |
Inatumika |
2.
|
Computer (Desktop)
|
1 |
Nzima |
Inatumika |
3.
|
Blower
|
1 |
Nzima |
Inatumika |
4.
|
Cable strippers
|
2 |
Nzima |
Inatumika |
Vifaa vilivyopo havitoshi na hivyo vinaathiri sana utekelezaji wa majukumu, kitengo kimeweka katika mpango wa bajeti ya 2017/2018 kunnua vifaa vya ofisi na vitendea kazi.
UTEKELEZAJI NA USIMAMIZI WA MIRADI
Kitengo kinaendelea na jukumu lake la kusimamia na kutekeleza miradi ya Miundombinu ya Ndani ya Kompyuta (LAN).
Mradi wa Ufungaji wa Miundombinu ya Ndani ya Kompyuta (LAN ) katika Jengo la
Kituo Kimoja cha Biashara
Mradi huu umetekelezwa na umekamilika kwa gharama ya Tsh: 7,732,000/= (Milioni saba laki saba na elfu thelathini na mbili tu) ambazo zilifadhiliwa na Local Investment Climent Project (LIC). Mradi huu ulianza Mwezi Desemba, 2016 na kukamilika mwezi Januari, 2017.
Mafanikio, Changamoto na Mikakati
Mafanikio
Kuwezesha kutoa taarifa sahihi na za haraka za kifedha za ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mifumo ya mapato (LGRCIS) na matumizi (EPICOR 09).
Kutoa risiti na nyaraka mbalimbali za kifedha zinapohitajika.
Kufuatilia na kuangalia mapato yaliyokusanywa kwa kutumia POS zilizogawanywa kwa watendaji.
Kuthibiti au kupunguza makosa yaliyojitokeza katika ukusanyaji wa kawaida kwa kutumia vitabu .
Kuwawezesha walipa bili kulipa na kuangalia bili zao za huduma mbalimbali kama vile leseni za biashara, kwa kutumia simu za kiganjani iliyounganishwa na NMB mobile kwa kuwa LGRCIS (Local Government Revenue Collection Information System) imeunganishwa na CCS (Cash Collection System).
Kutunza kumbukumbu za mapato na taarifa za walipa bili.
Kupungua kwa vifaa vya TEHAMA visivyofanyakazi kwa kuwa matengenezo huwanywa mara kwa mara.
Kuongezeka kwa ustadi wa watumiaji wa kompyuta na mifumo ya kompyuta baada ya kutoa maelekezo sahihi ya utumiaji wa kompyuta kwa watumiaji hao.
Kupungua kwa changamoto za upotevu wa taarifa miongoni wa watumiji wa kompyuta.
Changamoto
Mikakati ya kupambana na Changamoto
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.