KILIMO CHA KOROSHO
Katika msimu wa Kilimo 2016/17 Halmashauri ya Wilaya imeendelea kuongeza uzalishaji wa miche ya korosho, usambazaji wa mbegu na utunzaji wa miche iliyokwisha pandwa katika misimu mingine iliyopita.Katika msimu wa 2016/17 Halmashauri kwa kushirikiana na Bodi ya korosho wamezalisha miche 63,000 na kuisambaza kwenye vijiji 12 vya Mazae, Berege, Chitemo, Chinyika, Lukole, Kingiti, Iyenge,Nghambi, Kibakwe, Ikuyu, Pwaga na Idilo na Jumla ya kilo 110 zimesambazwa kwenye vijji vya Mazae, Igoji II, Mazae, Chamanda na Iwondo.
Katika msimu wa 2017/18 Wilaya inampango wa kuzalisha miche 600,000 ya mikorosho kwa kushirikiana na bodi ya Korosho.Miche ya mikorosho itazalishwa na jumla ya vikundi 9 ambavyo vimeshaanza maandalizi ya kuzalisha.
Vijiji ambavyo vipo kwenye mpango wa kuendeleza zao la korosho msimu wa 2017/18.
Ni kama ifuatavyo: Ilolo, Mazae, Kisokwe, Idilo, Chunyu, Nghambi, Kazania, Berege, Chitemo, Sazima, Igoji I, Chinyika, Igoji II, Vinghawe, Kimagai, Inzomvu, Pwaga, Godegode, Kingiti, Lukole, Iyenge, Kibakwe na Ikuyu.
Kwa Taarifa zaidi pakua nyaraka hizi hapa chani:
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.