Historia
Jiografia ya wilaya ya Mpwapwa
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ni miongoni mwa Halmashauri nane (8) za Mkoa wa Dodoma. Makao makuu yapo umbali wa km.120 kutoka makao makuu ya Mkoa wa Dodoma.
Halmashauri ipo kati ya latitude 6°00” na 7°00” Kusini mwa mstari wa Ikweta na Longitudo 35°45” na 35°00” Mashariki mwa mstari wa ‘Greenwich’.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwa upande wa kaskazini, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa upande wa magharibi. Upande wa mashariki inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa (mkoa wa Morogoro) na kusini inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa (Mkoa wa Iringa).
Ukubwa wa eneo
Wilaya ina eneo la kilometa za mraba 7,479 sawa na (18.35%) ya eneo lote la Mkoa wa Dodoma. Eneo hili ambalo ni sawa na hekta 737,900 linatumika kwa shuguli za kilimo, ufugaji, hifadhi ya misitu na makazi
Muundo wa Halmashauri ya Wilaya Kiutawala
Halmashauri ya Wilaya ina Majimbo 2 ya Uchaguzi, Tarafa 4, Kata 33, Vijiji 113, Vitongoji 575 na Mitaa 18.
Idadi ya Watu
Kutokana na Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Halmashauri ya Wilaya ilikadiriwa kuwa na wakazi 305,056 ambapo Wanaume wakiwa 147,306 (48.3%), Wanawake 157,750 (51.7%) na Kaya 66,316. Aidha, kwa mwaka 2016 kwa kutumia ukuaji wa asilimia 2.1, inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 331,500 kati yao Wanaume 162,435, na Wanawake 169,065 wanaoishi katika Kaya 72,065. Mgawanyo wa idadi ya watu kitarafa kwa ulinganisho wa Idadi ya Watu Matokeo ya Sensa ya Mwaka 2012 na makadirio ya watu mwaka 2016
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.