USAFI WA MAZINGIRA
Halmashauri kupitia Idara ya usafi na Mazingira inaendelea kusimamia utunzaji na udhibiti wa uharibifu wa mazingira ndani ya wilaya. Hadi sasa watuhumiwa 65 wamebainishwa na kuthibitika kufanya uharibifu wa mazingira kati yao watuhumiwa 8 wamelipa faini tayari na watuhumiwa 2 wamefungwa gerezani. Pamoja na hatua hizo bado taratibu za kuwafikisha kwenye mabaraza ya kata watuhumiwa waliobaki zinaendelea na ufuatiliajiunaendelea.
Uzoaji wa taka ngumu – juhudi kubwa zimefanywa na idara kuhakikisha taka zote zinazozalishwa zinakusanywa na kusafirishwa, kutumia gari la Halmashauri na magari ya wadau mbalimbali wa Halmashauri.
Halmashauri inaendelea kusimamia usalama wa afya mazingira na kudhibiti milipuko ya magojwa itokanayo na uchafu wa mazingira.
MAJUKUMU YA IDARA KWA UJUMLA
HALI YA WATUMISHI
Idara ina jumla ya watumishi 11 wa kada mbili, watumishi 9 kutoka kitengo cha Usafi na 2 kitengo cha Mazingira.
Jedwali No. 1 WATUMISHI
NA
|
KADA
|
MAHITAJI
|
WALIOPO
|
UPUNGUFU
|
1
|
MKUU WA IDARA
|
1
|
1
|
0
|
2
|
USAFI
|
36
|
9
|
27
|
3
|
MAZINGIRA
|
36
|
2
|
34
|
MUUNDO WA IDARA
Idara ya Usafi na Mazingira imegawanyika katika vitengo viwili yaani kitengo cha USAFI na kitengo cha MAZINGIRA.
Kitengo hiki kina wajibika kutekeleza majukumu mbalimbali kama ifuatavyo
B: KITENGO CHA USAFI NA AFYA YA JAMII
Kitengo cha usafi na afya ya jamii kina majukumu yafuatayo
MIKAKATI YA IDARA
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kupitia Idara ya Usafi na Mazingira imejiwekea mikakati mbalimbali ili kuboresha utunzaji wa mazingira na afya ya jamii. Mikakati hiyo ni pamoja na;-
1. Kuhakikisha kwamba elimu juu ya Hifadhi ya mazingira na afya ya jamii kwa wadau mbalimbali inafanyika mara kwa mara ilikupunguza au kuondoa kabisa tatizo la uharibifu wa mazingira magonjwa ya milipuko katika Wilaya.
2. kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa mazingira no 20 ya 2004 na marekebisho yake ya 2016 dhidi ya waharibifu wa mazingira, na ukiukwaji wa sheria ya afya ya jamii na 1 ya 2009 dhidi ya wale wote wanaoenda kinyume na kanuni, taratibu na miongozo ya afya ya jamii.
3. Kufuatilia na kuainisha maeneo yanayopaswa kuhifadhiwa kama maeneo yenye chepechepe za maji (Aridhi oevu), kandokando mwa kingo za mito, milima ya hifadhi ya jamii, na maeneo mengine yenye thamani mbalimbali ya uhifadhi.
4. Kuboresha taaluma ya watumishi pamoja na maslahi.
5. kuandaa mikakati na mipango mbalimbali ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira kama programu za upandaji miti.
6. kufuatilia maandalizi, mapitio na vibali vya Tathmini za athari za mazingira zina fanyika kwa miradi mikubwa ya uwekezaji kama vile miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji, Mashule, Minara, uchimbaji wa madini na pia wachimbaji wadogo wa madini kuhakikisha wa mipango ya ulinzi wa mazingira (EPP) na mipango ya usimamizi wa mazingira yaani (EMP) kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa Mazingira na 20 ya 2004 na sheria ya madini na 14 ya 2010.
7. Kuunda kamati za kuhifadhi mazingira kuanzia ngazi ya vijiji,kata na wilaya pamoja na klabu za mtoto kwa mtoto mashuleni.
8. Kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi kwa viongozi, watendaji na kamati za Mazingira.
9. Kutoa Elimu ya afya katika jamii, juu ya kanuni za afya, ujenzi wa vyoo na unawaji mikono, ukusanyaji wa taka Ngumu na za hatari katika maeneo yao, athari za bidhaa zilizokwisha muda wake na usafi wa maeneo ya kutolea huduma kama vile bucha, maduka nyumba za wageni nyumba za kuishi, zahanati , shule, vyuo mashine za nafaka,na migahawa.
10. kuandaa maandiko mbalimbali yanayohusu uhifadhi wa mazingira na afya ya jamii ndani ya Wilaya ya Mpwapwa.
BAADHI YA SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA WANCHI WA MPWAPWA KUHARIBU MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI
Pic: Uharibifu wa mazingira kwa shughuli za kilimo na mifugo safu za milima wotta kijiji cha Mzase kata ya berege
Pic:Usimamizi na utoaji elimu kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji kitogoji cha kwamdyanga Mpwapwa mjini safu za milima Kiboriani (kwamdyanga water intake)
Pic: kiwanda kidogo cha uchenjuaji wa kopa katika machimbo ya madini ya kopa Tambi kata ya Matomondo (ushauri kuhusu uandaaji wa mipango ya ulinzi wa mazingira – EPP na EMP)
Pic: madini ya kopa yaliyochimbwa tayari kwa usafirishaji katika machimbo ya Tambi kata matomondo
Pic: Mgodi wa machimbo ya kopa Tambi kata ya matomondo
Pic : machimbo ya Kopa katka mgodi wa Rudi kata ya Rudi
Pic: utoaji wa elimu kuhusu uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji ( WDC 2 za Kingiti na Mwanawotta) zilikutanishwa katika chanzo cha maji ili kujionea uharibifu na kupewa elimu ya uhifadhi na Afisa mazingira pamoja na Mhandisi wa Maji Mpwapwa.
Pic : kamati ya mazingira Kijiji cha Mtamba Kata ya Rudi.baada ya kufanya ukaguzi wa maeneo ya hifadhi za milima na vyanzo vya maji Pamoja na afisa Mazingira Mpwapwa watatu toka kushoto.
Pic : maeneo ya milima na vyanzo vya maji Kijiji cha Mtamba Kata ya Rudi yaliyoharibiwa na kulimwa kilimo cha ufuta.
Pic: Uwezeshaji wa kamati ya mazingira kijiji cha Mtamba Kata ya Rudi chini ya Afisa Mazingira na Afisa afya mazingira watatu toka kulia.
Pic: shuguli za kulinda na kutoa elimu ya afya ya jamii, baada ya maafisa afya mazingira kukamata nyama isiyofaa kwa matumizi ya binadamu kwenye bucha. Pichani ni wanafunzi wa chuo cha mifugo Visele wakishuhudia utupwaji wa nyamba iliyokamatwa mabuchani Mpwapwa.
Pic: Shughuli za utekelezaji wa kampeini ya usafi wa mazingira(national sanitation campaign) kuhimiza ujenzi wa vyoo katika kijiji cha Kimagai kata ya Kimagai. Pichani ni zoezi la uchefushaji washiriki wakichora Ramani ya kijiji na kuonyesha maeneo ya vichaka na misutu watu wasio na vyoo wanakojisaidia
Uwekaji wa vifaa bora vya unawaji mikono katika taasisi na mashule na maeneo ya huduma za jamii za unawaji mikono (SARO TAP DESIGN)
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.