Ujenzi na Zimamoto
Wilaya inahudumia jumla ya km 1,098 zikigawanyika kati ya barabara za Wilaya (District roads) na barabara za vijiji (feeder roads). Serikali Kuu imeendelea kuzihudumia barabara kuu (Trunk roads) na za Mkoa (Regional roads) zipatazo km 346 zilizoko upande wa Wilaya ya Mpwapwa. Barabara hizo zinahudumiwa kupitia Wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Dodoma na zinaweza kupitika kwa kipindi cha mwaka mzima. Katika Barabara za Wilaya bado zinapitika vizuri kwa asilimia 80 japo upo uharibifu mkubwa unaojitokeza kutokana na mvua kubwa zinazonyesha na kusababisha makorongo makubwa yanayohitaji ujenzi wa vivuko. Wilaya inaendelea na jitihada za kuzifanyia matengenezo barabara za Wilaya na Vijiji kadiri fedha zinavyopatikana.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.