Mapato ya Ndani:
Halmashauri ya Wialaya ya Mpwapwa katika mwaka wa fedha 2015/2016 ilipanga kukusanya mapato ya ndani kiasi cha shilingi 1,420,483,574.00. Hadi kufikia mwezi Januari 2016 Halmashauri imekusanya jumla ya Shilingi 551, 692,282.21 sawa na asilimia 38.83
Jedwali No.13: Hali ya ukusanyaji wa Mapato ya ndani 2013/14 – 2015/16:
Mwaka |
Lengo |
Mapato halisi |
% ya mapato |
2013/2014
|
662,362,000.00
|
642,288,704.00
|
97 |
2014/2015
|
1,269,645,000.00
|
984,233,287.00
|
78 |
2015/2016
|
1,420,483,574.00
|
551,692,282.21
|
38.83 |
3.2 Changamoto:
Zifuatazo ni changamoto zilizojitokeza katika ukusanyaji wa mapato;
Ukame: Kukosekana kwa mvua za kutosha imesababisha ukame ulioikumba sehemu kubwa ya Wilaya yetu na kusababisha uzalishaji kupungua wa mazao, samaki katika bwawa la Mtera na hivyo kuathiri ushuru wa mazao na samaki kupungua. Pia ukame umeathiri shughuli za ufugaji, hivyo kupunguza mapato yanayotokana na mifugo.
Kumekuwa na ugumu wa ukusanyaji wa ushuru wa madini na kuwapata wachimbaji hao kwani wengi ni wadogowadogo na hawana ofisi hivyo ni vigumu kuwapata.
Kuchelewa kupitishwa sheria ndogo kumeathiri ukusanyaji wa mapato kwani ukusanyaji unatumia viwango vya zamani ambavyo havina tija.
3.3 Usimikaji wa Mfumo wa Kielectronic
Halmashauri imeshafunga mfumo wa kukusanyia mapato. Mfumo wa LGRCIS.
Utekelezaji
Mfumo wa LGRICS, utandazaji wa miundombinu umekamilika, sever zimewekwa, vifaa vimeshaunganishwa na mfumo umeanza kufanya kazi kwa kuanzia na makao makuu ya Halmashauri.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.