ARDHI NA MALIASILI
Utekelezwaji wa majukumu ya Idara ya Ardhi na Maliasili kwa sehemu kubwa unaongozwa na Sera, Sheria , Kanuni, miongozo na maagizo mbalimbali ya kiserikali. Sera hizo ni pamoja na Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 pamoja na sheria zake, Sheria Namba 4 na 5 ya mwaka 1999, Sheria ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi ya mwaka 200, Sheria ya Mipango miji ya Mwaka 2007. Sekta ya Misitu inaongozwa na Sera ya Taifa yaMisitu ya Mwaka 1998 na sheria yake Na. 14 ya Mwaka 2002 Sekta ya Wanyamapori inaongozwa na Sera ya Wanyamapori ya Mwaka 2007 na sheria yake Namba 5 ya Mwaka 2009 Aidha Idara inatumia Sera na Sheria zingine Mtambuka zinazotumika nchini zinazohusu masuala ya Ardhi na Maliasili.
Hivyo idara iantekeleza majukumu yake katika maeneo makuu mawili ambayo ni usimamizi wa maenedeleo ya ardhi na Maliasili. Utekelezaji wa shughuli hizo unafanyika kupitia vitengo vifuatavyo;
Ardhi Utawala
Kitengo hiki hufanya utekelezaji wa zoezi la kuandaa miliki za viwanja na mashamba yaliyopimwa,kuandaa vyeti vya ardhi vya vijiji, kutatua migogoro mbalimbali inayotokea miongoni mwa makundi yanayotumia Ardhi, kukusanya kodi ya Ardhi, kutunza kumbukumbu za miliki na kutekeleza miamala mbalimbali ya ardhi kama vile kutengua miliki na kuhamisha miliki.
Upimaji na Ramani
Kitengo hiki hushughulika na upimaji wa viwanja na mashamba, upimaji wa vijiji, upimaji wa maeneo mbalimbali kutokana na maelekezo ya kiserikali na uwekaji wa alama za rejea za upimaji.
Mipango Miji.
Kitengo hiki hushughulikia uandaaji wa mipango ya miji na vijiji, mipango hii hujumuisha;
Misitu.
Kitengo hiki kinashughulika na uhifadhi wa misitu, uendelezaji wa misitu na matumizi endelevu ya misitu na ukusanyaji wa maduhuli yatokanayo na mazao ya misitu. Wilaya ya Mpwapwa ina hifadhi 3 za Misitu ya Serikali, Hifadhi hizo ni pamoja naMafene, Wotta na Mang’aliza.
Pia kwa sasa Wilaya inapendekeza msitu wa Kiboriani kuwa Hifadhi ya Msitu wa serikali. Aidha kuna misitu ambayo ipo chini ya vijiji vilivyopimwa nayo ni; Mwenzele, Mwanawota, Rufu, Rufusi,Mima, Iyenge, Bumila, Tambi, Mbori, Mbuga,Galigali,Matonya, Lwihomelo, Kizi,Kingiti, Kati ya misitu hiyo misitu ya PFM ni saba na ambayo imetokana na Mpango wa matumiazi bora ya Ardhi (Land use plans) ni misitu sita, Misitu miwili ni ya kawaida
Wanyama Pori
Kitengo hiki hushughulika na hifadhi ya wanyapori, uemdelezaji, na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali yatokanayo na wanyamapori. Wilaya ya Mpwapwa ina pori tengefu moja ambalo ni Rudi (Rudi Game Controlled Reserve) ukubwa wa eneo ni hilo ni Hekta 136,450. Aidha pori hili lina hifadhi ya wanyama mbalimbali kama fisi,swala,na digidigi, wanyama wengine kama tembo huja na kuondoka.
Nyuki
Kitengo hiki hushughulika na zoezi la maendeleo ya ufugaji wa nyuki na uvunaji wa asli n anta. Katika Wilaya ya Mpwapwa shughuli za hizo zinafanyika katika
Vikundi 41 na Mwananchi mmoja mmoja, Wilaya ina jukumu la kusimamia ufugaji nyuki katika vikundi na wananchi kwa ujumla.
Uthamini
Kitengo hiki hushughulika na uthamini wa malengo mbalimbali, uthamini huo hulenga Mizania, kuhamisha miliki, fidia, makadirio ya kodi ya ardhi na majengo, uhamisho wa miliki na kujua thamani ya soko.
Hifadhi ya milima ya Rubeho
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.