Ufugaji sehemu kubwa ni huria, na wanyama wafugwao kwa kiasi kikubwa ni wa asili ambao wanakadiriwa kuwa ngombe 179,737, mbuzi 148,317, kondoo 56,343, Punda 3,262 na kuku 204,923 Inakadiriwa kuwa mifugo inachangia karibu asilimia 45 ya pato la Wilaya.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ina eneo la ardhi lenye ukubwa wa hekta 228,991 linalofaa kwa kilimo na kati ya hizo hekta 142,277 ndizo zinazotumika. Kati ya eneo linalofaa kwa kilimo, hekta 5,726 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji na zinazotumika ni hekta 2,661. Hekta 262,000 zimetengwa kwa ajili ya ufugaji. Eneo hili ni moja ya fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa mazao ya chakula, biashara na ufugaji.
Uzalishaji wa maziwa kwa wastani unakadiriwa kuwa lita moja kwa ng’ombe wa kienyeji japokuwa kwa hali ya kawaida ng’ombe mmoja wa maziwa anatakiwa kuzalisha angalau lita sita kwa siku. Changamoto zinazojitokeza kutofikia uzalishaji wa lita sita kwa siku ni pamoja na malisho hafifu na yasiyobora, magonjwa, utunzaji usio bora wa mifugo na aina ya ng’ombe.
Mikakati
mikakati iliyopo na endelevu ni kutoa elemu kwa wafugaji namna ya ufugaji bora na wenye tija. Kudhibiti magonjwa ya mlipuko na yale yanayojitokeza mara kwa mara kwa kutoa chanjo kwa ajili ya kinga na tiba. Tunaendelea kutoa elimu pia juu ya malisho bora yanayofaa kwa mifugo na kuhamasisha upandaji wa malisho.
Ubora wa mifugo ni mdogo kutokana miundombinu michache kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mifugo. Magonjwa yanayoshambulia na kuzuru afya za mifugo hivyo kupunguza uzalishaji na ubora wa nyama na maziwa. Utoaji wa huduma za ugani kwa mifugo unategemea zaidi uwepo wa miundombinu kama majosho, vituo vya afya ya mifugo na nyanzo vya maji hali halisi ya miundo mbinu ya mifugo imeainishwa kwenye jedwali Na.1
Jedwali Na.1: Hali ya miundombinu ya mifugo Mwaka 2016
S/N
|
Miundo mbinu |
Hali halisi |
|||
Mahitaji |
iliyopo |
Upungufu
|
Maelezo |
||
1 |
Majosho
|
50 |
33 |
18 |
27 yanatumika, 6 yanahitaji ukarabati
|
2 |
Minada
|
16 |
16 |
0 |
Inafanya kazi
|
3 |
Vituo vya Tiba
|
5 |
3 |
2 |
Ukarabati unahitajika
|
4 |
Krash
|
84 |
12 |
72 |
3 vinafanya kazi, 9 vinahitaji ukarabati
|
5 |
Machinjio
|
5 |
1 |
4 |
Inafanya kazi lakini inahitaji ukarabati
|
6 |
Majengo ya Kulainisha ngozi
|
8 |
4 |
4 |
Yote yanafanya kazi
|
7 |
Malambo (Charcol dam)
|
44 |
20 |
24 |
Malambo hayatoshelezi
|
8 |
Mabirika ya kunywea Mifugo (Water troughs)
|
50 |
14 |
36 |
Zote zinafanya kazi
|
9 |
Vijiwe vya Kuchinjia Mifugo
|
10 |
4 |
6 |
Havitoshelezi
|
Wilaya inanufaika na bwawa la Mtera lenye Ukubwa wa km 640. Bwawa hili linazalisha samaki na umeme. Mapato yatokanayo na shughuli za uvuvi ni kati ya asilimia 4 hadi 5 ya mapato yote.
Shughuli nyingine za ufugaji wa samaki zinazoendelea katika mabwawa madogo madogo katika kata za Wotta na Mpwapwa ambapo yapo mabwawa 26 ambayo yamefugwa samaki aina ya sato (Oreachranis nilotica). Mabwawa haya yanasaidia sana upatikanaji wa kitoweo kwa jamii katika maeneo haya.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.