Kazi Za idara hii
a.Kutekelea sheria na sera na kushauri masuala mbali mbali yahusuyo Maji.
b.Kufanya Tafiti na kufanya ukagui wa maji safi na salama.
c.Kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maji katika kuboresha huduma ya utoaji maji katika wilaya.
d.Kujenga uwezo katika kupanga, kutekelea na kusimamia miradi ya maji kwa kutumia teknolojia rahisi inayokubalika katika ngazi ya jamii.
e.Kuandaa mipango na Bajeti katika miradi ya Maji.
f.Kuwajengea uwezo wana jamii ili wawezekuendsha miradi ya maji
g.Kukarabati na kujenga miundombinu ya Maji.
h.Kushauri mamlaka za juu ili ziweze Kutoa fedha kwaajili ya miradi ya maji kufuatia juhudi zinazoonyeshwa na wananchi.
i.Kuandaa makadirio ya gharama za ujenzi wa miradi ya maji.
j.Kuandaa tarifa za idara za utekelezaji wa miradi ya maji katika kipindi cha robo, na mwaka.
Hali ya Upatikanaji wa Maji Wilayani.
Wilaya ya Mpwapwa ina jumla ya vyanzo vya maji vipatavyo 247, ikiwemo maji ya mtiririko 32, visima virefu vipo 43, visima vifupi 144, matenki ya kuvunia maji ya mvua 43, uboreshaji wa chemichemi 28. Hata hivyo ni vyazo 232 ndivyo vinavyofanyakazi .Idadi ya watu wanaopata maji safi na salama ni 184,010 sawa na asilimia 56.8 ya makadirio ya watu wapatao 323,947.
Watu 142,375 kati ya watu 282,312 waishio vijijini sawa na 50.4% wanapata maji safi. Utekelezaji wa miradi ya maji chini ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) kwa miradi ya vijiji vine ya Chinyanghuku, Kimagai, Chunyu na Kisima umekamilika,
Mkakati wa uvunaji maji ya mvua unaendelea kutekelezwa, unoahusisha kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uvunaji wa maji ya mvua, ushirikishaji wa wadau mbalimbali katika kuboresha na kuwezesha kutekeleza mpango kwa pamoja na kuwafikia wananchi wengi. Aidha mkakati unahusisha ujenzi wa miundo mbinu ya kuvunia maji ya mvua (matanki na mabwawa) katika vijiji 113 na taasisi, utekelezaji wake ulianza mwaka 2011/2012
Aidha Halmashauri inaendelea kuhakikisha kuwa;
Maadhimisho ya kilele ya Wiki ya Maji Katika Wilaya yaliyofanyika tarehe 23.03. 2017 Katika Kata ya Chitemo.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.