(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Kamati ya Ulinzi wa Mwanamke na Mtoto ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa leo imefanya kikao chake cha pili katika Ukumbi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira uliopo katika jengo la Mamlaka hiyo Wilayani Mpwapwa. Kikao hicho kimefanyika chini ya Mwakilishi wa Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndug. Khamlo Njovu amabye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akimwakilisha mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Paul Mamba Sweya.
Katika kikao kazi hicho wajumbe walithibitisha agenda, kuthibitihsha muhtasari wa kikao cha kamati hiyo kilichopita cha tarehe 26 Septemba 2018, kujadili yatokanayo na kikao kilichopita cha tarehe 26 Septemba 2018, kupokea na kujadili kwa kina taarifa za wadau juu ya utekelezaji wa shughuli za ulinzi wa mwanamke na mtoto kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba 2018.
Taarifa toka Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF - Children's Dignity Forum): Kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba 2018, CDF imefanya shughuli zifuatazo:- kutoa mafunzo ya haki za watoto na stadi za maisha ambapo wasichana 480 walifikiwa kutoka shule 7 za Sekondari na ( za Msingi kutoka kata za Mpwapwa Mjini, Kibakwe, Pwaga na Berege; Kutoa mafunzo ya
ya uzazi kwa wasichana ambapo wasichana 155 walifikiwa kutoka katika shule 7 za Sekondari na 9 za Msingi kutka kata za Mpwapwa Mjini, Kibakwe na Berege; Kufanya Bonanza la michezo kuhamasisha ushiriki wa wanaume katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto ambapo waendesha bodaboda 20 (wanaume) nawanachama 48 (wanawake
8 na wanume 35) wa kikundi cha Malezi Berege walifikiwana mafunzo ya nafasi ya wanaume katika kukomesha ukatiliwa kijinsia na zaidi ya wananchi 400 walihudhuria bonanza hilo.
Pia kulikuwa na shughuli ya kufanya mkutano wa mwaka wa Wilaya wa wadau wa Haki za Mtoto WIlayani Mpwapwa ambapo wajumbe 49 (wanawake 29 na wanaume 20) walihudhuria na kujadili hali ya ulinzi wa mtoto kiwilaya, changamoto na ukatili dhidi ya watoto pamoja na kuweka mikakati ya kukabiliana na aina zote za ukatili wa watooto. Aidha kulikuwa na kushiriki kongamano la Kitaifa la kukabiliana na ndoa za utotoni, mimba za utotoni, ukeketaji; pia kulikuwa na kongamano la Sauti za Wanawake (Girls Voice Forum) ambapo jumla wasichana 10 kutoka Mpwapwa walishiliki kongamano hilio la kitaifa lililofanyika Dae r es salaam. Pia jumla ya wasichana 20 walihudhuria kongamano la Sauti za Wasichana lililofanyika Chuo Kikuu cha Ualimu Dar es salaam (DUCE).
Afisa Maendeleo ya Jamii Ndug. Magnus Mpangala (Kulia) akiwasilisha taarifa ya CDF.
Taarifa Toka Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia: taarifa hii ni ya kuanzia mwezi Januari hadi Novemba 2018 ambapo kuna kesinyingi zimeripotiwaza makosa ya unyanyasaji wa kijinsia katika kituo cha Polisi Wilaya ya Mpwapwa kama inavyoonyesha katika jedwali hapa chini:-
Askari Polisi anayeshughulikia Dawati la Jinsia Ndug. Magreth Lyaro (wa kwanza kulia) akiwasilisha taarifa ya Dawati la jinsia toka Polisi Mpwapwa
Taarifa toka idara ya Elimu Sekondari: Idara ya Elimu Sekondari inasimamia na kuratibu shughuli zote za Elimu Sekondari katika Wilaya ya Mpwapwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha watoto wa kike na wakiume waliochaguliwa kujiunga na shule za sekondari wanapata haki ya kumaliza Elimu ya Sekondari. Shule za Sekondari za Halmashauri ya WIlaya ya Mpwapwa zina jumla ya wanafunzi 10,224 (wasichana 5,200 na wavulana 5,024) kwa mujibu wa takwimu za wanafunzi wote za mwaka 2018. Kuna sababu nyingi zinazofanya kuwepo na mdondoko kwa wanafunzi wa wetu ambazo ni mimba kwa watoto wa kike, utoro sugu, ugonjwa, kufukuzwa shule kutokana na utovu wa nidhamu. Kwa kipindi cha mwaka 2018 jumla ya wanafunzi 566 (wasichana 230 na wavulana 336) wameacha shule kwa kipindi cha mwaka mmoja kama inavyoonyesha katika jedwali:-
Afisa Elimu Sekondari Ndug. Honorata Kabunduguru (kulia) akiwasilisha taarifa ya Elimu sekondari
Taarifa toka Mahakama Maalum ya Watoto:- Mahakama ya watoto ni Mahakama iliyoanzishwa kutokana na sheria ya mwaka 2009 kwa maagizo ya Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Tanzania kuwa mahakama ya mwanzo ya Mpwapwa Mjini imeteuliwa kushughulikia mashauri ya watoto. Katika kumlinda mtoto kisheria mahakama ya watoto inapaswa iwe na muonekano tofauti na mahakama zingineza mwanzo au za wilaya. Hapatakiwi awepo askari mwenye kuvaa sare au Afisa wa Mahakama mwenye kuvaa mavazi ya kutisha.
Wakati wote wa uendeshaji wa Mahakama hizo maafisa wa Ustawi wa Jamii wanatakiwa wawepo na wengine wanaotakiwa kuwepo ni pamoja na Mheshimiwa Hakimu Mkaazi, Mwendesha mashtaka, mzazi au mlezi wa mtoto na mkao wake uwe wa majadiliano (Mduara) ili kuweza kuondoa hofu kwa mtoto. Afisa Ustawi anatakiwa awepo Mahakamani wakati wote kwa lengo la kumlinda mtoto na kuandaa na kuwasilisha taarifa ya uchunguzi ya kijamii ya mtoto mahakamani.
Mashauri yaliyofikishwa katika mahakama ya watoto katika Wilaya ya Mpwapwa kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba 2018 in kama ifuatavyo:- Ubakaji mashauri 5 yametokea Vighawe, Kisisi, Mima, Ilolo na Kidabaga; mashauri ya wizi ni shauri 1 kutoka Majengo - Mpwapwa Mjini, Wizi wa Mifugo shauri 1 lililotokea Chitemo, shauri 1 la utoaji mimba lililotokea kijiji cha Mgoma na Shambulio la kudhuru mwili shauri 1 lililotokea Ilolo.
Afisa Ustawi wa Jamii Ndug. Anthony Mbabile (wa kwanza kulia) akiwasilisha taarifa toka Mahakama ya Watoto Mpwapwa
Maazimio ya Kamati ya Ulinzi wa Mwanamke na Mtoto Wilaya ya Mpwapwa
1. TAYOA wanatakiwa kuandaa na kuwasilisha kwa kamati taarifa yao ya utekelezaji wa shughuli zao kuanzia Oktoba hadi Disemba 2018 kwa kuwa hawajawasilisha taarifa yao, wakati wao pia ni wdau wa ulinzi wa mwanamke na mtoto. Taarifa hiyo iwasilishwe katika kikao kijacho cha Aprili 2019.
2. Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa na Afisa Biashara, wafuatilie na kukagua leseni za maduka ya dawa na kufanya ukaguzi ili kubaini kama kuna maduka yanauza dawa za kutoa mimba wanazozitumia wanafunzi kutoa mimba.
3. Kamati inashauri Serikali ijenge mabweni katika shule ili wanafunzi na hasa wasichana waweze kukaa hosteli kwa kuwa jiografia ya Mpwapwa sio rafiki na shule nyingi zipo umbali mrefu kutoka makazi ya watu hivyo huwalazimu wanafunzi kutembea umbali mrefu kutoka nyumbani hadi shuleni.
4. Kamati inashauri serikali ijenge shule mpya katika maeneo ambayo kata tatu zinashirikiana shule moja ya sekondari mfano: Shule ya Sekondari Mima.
5. Wazazi wafuatilie mienendo ya watoto wao toka nyumbani hadi shuleni na kukagua madaftari ya watoto wao.
6. Kuwabana wanafunzi wa kike waliopata mima ili kuwataja walipa mimba ili wawataje waliowapa mimba ili watiwe hatiani na baadae kufungwa miaka 30 na kuwa fundisho kwa wengine.
7. Afisa biashara kwa kushirikiana na vyombo vya dola kukagua nyumba za kulala wageni ili kubaini kama kuna wanafunzi na watoto wanalala kwa lengo la kufanya ngono.
8. Watendaji wa kata kufuatilia na kuzuia uwepo wa miziki au ngoma zinazokesha (vigodoro) na vibanda vya video kwa kuwa haviruhusiwi kisheria.
Kwa taarifa zaidi pakua nyaraka hizi:
MUHTASARI WA KIKAO CHA KAMATI YA ULINZI WA MWANAMKE NA MTOTO TAREHE 26-09-2018.docx final.pdf
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.