Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amewaalika LEAD Foundation kuja wilayani Mpwapwa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kutoa elimu kwa wajumbe wa kamati hiyo juu ya kupanda miti na kutunza mazingira katika kuhamasisha program ya Kisiki Hai.
LEAD (Leadership Environment Action for Development) Foundation ni wadau wa utunzaji wa mazingira na wanafadhiliwa na mashirika mbalimbali ikiwemo Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). LEAD imeanzisha program ya utumzaji wa mazingira katika wilaya ya Mpwapwa katika kata za Rudi na Mpwapwa mjini ambapo vijijini 54 vitafikiwa na mradi huu kwa kaya 37,000 na kupanda miti ipatayo 2,960,000 ili kufikia lengo la kuwa na Dodoma ya kijani chini ya kauli mbiu ya Kijanisha Dodoma Iwe Poa. Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri (katikati) akifungua kikao cha DCC. (Picha na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa amezindua mradi huu kuanza kufanyakazi wilayani Mpwapwa ili kuifanya Mpwapwa kuwa ya kijani kwa kuanza na kata hizo mbili zilizotajwa hapo juu.
Mafunzo ya awali juu ya utunzaji wa mazingira yametolewa leo katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa kwa wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya na wamjumbe wote kwa ujumla wameupokea mradi na wameruhusu ufanyekazi katika Wilaya ya Mpwapwa. Pia Mkuu wa Wilaya amehaidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha azima ya Dodoma ya Kijani. Vile vile LEAD Foundation katika malengo yao wameweka mkakati wa kuhamasisha upandaji wa zao Mkakati la Kibiashara ambalo ni zao la Korosho kwa jina maarufu Dhahabu ya Kijani.
Wajumbe wa DCC wakifuatilia kwa umakini mafunzo juu ya utunzaji wa mazingira (Picha na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Pia katika kikao hicho cha DCC wajumbe waliwasilisha mada zinazohusu Elimu Msingi, Elimu Sekondari, Afya, Mazingira, Mipango, Mapato na Matumizi, Ardhi Kilimo cha Korosho na Viwanda, ambapo mjadala wa pamoja kwa kuwashirikisha LEAD Foundation ulifanyika na kiongozi wa foundation hiyo Askofu Mstaafu wa Kanisa la KKKT Ndug. Chiwanga amehaidi kuzifanyika kazi hasa changamoto za utunzaji wa mazingira kwa kuwapa wananchi elimu ya namna ya kutunza mazingira. Pia ameongeza kuwa program hii ni endelevu na kwa Mkoa wa Dodoma itakuwa kwa muda wa miaka 4.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri (katikati) akizindua program ya Kisiki Hai katika kikao cha DCC. (Picha na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Katika kikao hiki cha DCC wajumbe walipendekeza kauli mbiu ambayo itahamasisha wananchi na wadau wengine kuwekeza kwa wingi na kukuza uchumi wa wilaya ya Mpwapwa katika viwanda , madini na kilimo. Kauli mbiu hiyo ni "INUKA, TUIJENGE MPWAPWA MPYA"
Kwa taarifa ya kina pakua nyaraka hii hapa chini:
KISIKI HAI PROGRAM PRESENTATION.pdf
MCHAKATO WA KUCHAGUA WAWEZESHAJI WANNE WA KISIKI HAI KILA KIJIJI.pdf
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.