(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri ameitisha kikao cha pamoja cha Baraza la Biashara na Baraza la Madiwani ili kupanga na kujadili kwa kina mikakati ya namna ya kuendesha Baraza la Biashara la Wilaya ya Mpwapwa bila kutengemea wafadhiri. Wazo hili limejili kwa kuwa mfadhiri mkuu wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Mpwapwa ni Mradi wa LIC (Local Investment Climate Project) na hivi sasa muda wa mradi huo kufanyakazi nchini unaenda kuisha hivyo kama Baraza linatakiwa kujiwekea mikakati ya kujitengemea.
Wajumbe wa Baraza la Biashara wakiwa katika kikao cha pamoja na Baraza la Madiwani katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa
Katika hotuba yake ya Ufunguzi wa kikao hicho Mkuu wa Wilaya amewataka wajumbe kujikita kujadili na kufikiria kwa kina kuwa tutawezaje kujitegemea na kufashughuli za baraza kama kununua mbegu za korosho, kuendelea kujenga miradi mbalimbali, kuandika maandiko, kumlipa mshahara mratibu wa baraza la biashara na shughuli zingine bila ufadhiri.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Shekimweri ametoa fursa ya wajumbe kupitia muhtasari wakikao kilichopita cha tarehe 9/02/2018 katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya, kupata majibu ya yatokanayo na kikao cha tarehe 9/02/2018, kufuatilia na kusikiliza kwa umakini uwasilishwaji wa mpango na bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa mwaka 2019/2020 hadi 2021/2022 kwa sekta ya Kilimo, Mifugo na Ardhi; ambapo sekta ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika imetenga Tsh. 50,000,000.00 sekta ya Mifugo na Uvuvi imetenga Tsh. 81,909,180.00 na sekta ya Ardhi imetenga Tsh. 60,000,000.00 na kufanya bajeti yote katika sekta hizi tatu kuwa Tsh. 191,909,180.00.
Wajumbe wa Baraza la Biashara wakiwa katika kikapo cha pamoja na Baraza la Madiwani katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa
Pia wajumbe wamepitia utekelezaji wa maazimio na mpango kazi wa baraza la biashara kwa mwaka 2019, ambapo katika mpango kazi huo wajumbe wamependekeza kuongenzwe shughuli za Kutafuta masoko ya mazao, kuandaa sera ya uwekezaji ya Wilaya na ujenzi wa mabwawa ya umwagiliaji.
Kikao hicho cha baraza la biashara pamoja na baraza la madiwani kimeazimia kuwa kuundwe mfuko maalam wa Baraza la Biashara, Sekta ya umma na binafsi wachangie katika uendeshaji wa shughuli za Baraza la Biashara, umuhumi wa kuwa na baraza la biashara baada ya wafadhiri muda wao kuisha, kuwepo na mfumo huru wa uchangiaji kibajeti katika shughuli za baraza la biashara, kiundwe kikosi kazi kidogo ili kushauri namna ya uchangiaji na halmashauri iendelee kutenga fedha kwa ajili ya shughuli za baraza la biashara ili kuvutia uwekezaji katika Wilaya yetu.
Wajumbe wote kwa pamoja wameafikiana maazimio yote yaliyojadiliwa na kufikia muwafaka.
Kwa taarifa zaidi pakua nyaraka hizi:
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.