Mkurugenzi Mtendaji Bi Mwanahamisi H Ally amefanya kikao na wataalamu wa ujenzi wa Ofisi ya halmashauri ya Wiaya ya Mpwapwa katika eneo la mradi ùnapoendelewa kujengwa Juni 19,2025.
Kikao hicho kilichojumuisha wataalamu kutoka halmashauri pamoja na wataalamu wa ujenzi wa Ofìsi hiyo kimefanyika Mmbuyuni eneo la ofisi hiyo inapojengwa.
Lengo la kikao hicho ni kupata uelewa wa hatua za mradi huo ulipofikia pamoja na kuelewa changamoto zinazoukamili mradi na kuweza kuupatia utatuzi,vilevile Mkuregenzi Mtendaji amewataka wataalam hawa waengeze vifaa vinavyokosekana na kupungua katika kazi hiyo na waongeze kasi ya ujenzi huo wa awamu ya mwanzo ili waendane sambamba na mkataba wao.
Mradi kwa awamu ya mwanzo utagharibu kiasi cha Sh.800,000,000.00 na kiwango walichofikia kwa sasa ni uwekaji nondo chini cha mashimo na umwagaji zege.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.