Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw Kaspar K.Mmuya amefanya ziara ya kikazi wilayani Mpwapwa leo Juni 20,2025.
Wakati wa ziara yake hiyo amekagua jengo la Maabara linaloendelea kujengwa katika Kituo cha Afya Kibakwe ambalo mpaka sasa limefikia asilimia 65 ya ujenzi wake ili liweze kukamilika.
Hata hivyo ametembelea jengo la mama na mtoto na kupata taarifa za utendaji kazi wa wodi hiyo ambayo tahmini inaonesha takribani mwaka mmoja sasa hakuna vifo vya mama na mtoto vilivyotokea kutokana na uboreshaji wa huduma za afya zilizoopo.
Bw.Mmuya amewataka wasimamizi wa mradi huo kuuthamini na kuhakikisha wanaulinda mradi huo vizuri kwani hakuna watumiaji wengine isipokuwa wao wenyewe. "Hakikisheni mnautunza na kuuthamini mradi ili uweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu" amesema Bw.Mmuya.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.