Wadau wa Water for People wamefanya kikao cha utoaji wa tathmini na takwimu ya kazi iliyofanyika katika kaya pamoja na Taasisi za Umma mbali mbali Juni 19,2025 katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya.
Water For People
Every one forever
Ilifanya kazi ya kuhakikisha Taasisi za Umma kama vile Shule na vituo vya kutolea huduma za afya vinapata huduma ya maji,usafi wa mazingira na usafi binafsi,katika upande wa jamii inahakikisha upatikanaji wa maji,huduma binafsi na usafi wa mazingira.
Kwa upande wa Forever ni kuhakikisha Wilaya na Jumuia kuwa na uwezo wa kuendeleza mifumo ya upatikanaji wa maji,usafi wa mazingira na usafi binafsi.
Bi Gundelinda ameelezea baadhi ya changamoto walizokutana nazo wakati wakitekeleza zoezi hili ikiwemo umbali wa maeneo lakini pia mvua zilizonyesha kusababisha uharibifu wa njia na kushindwa kuyafikia maeneo husika,na upimaji wa maji.
Kikao hicho cha Water For People kimehudhuriwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya Ndg Obert Mwalyego,Mkurugenzi Mtendaji Bi Mwanahamisi H Ally pamoja na wadau mbali mbali wa Halmashauri na Taasisi.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.