Na: Shaibu J. Masasi; Afisa TEHAMA - Mpwapwa Dc.
Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe ya Wilaya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Paul Mamba Sweya leo amefungua kikao cha robo ya tatu (2019/2020) ya kamati hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya na kuhudhuriwa na wajumbe wa kamati hiyo. Katika kikao hicho idara mtambuka zinazohusiana moja kwa moja na lishe zimewasilisha taarifa zake za utekelezaji wa shughuli za lishe kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2019/2020. Idara zilizowasilisha taarifa ni pamoja na: Idara ya Kilimo, Mifugo, Afya, Elimu Msingi, Elimu Sekondari na idara ya Usafi na Mazingira.
Katika taarifa iliyowasilishwa na Afisa Lishe wa Wilaya Ndugu. Asiatu Mmbwambo imeeleza kuwa kwa sasa utekelezaji wa shughuli za lishe umepanda toka 27% hadi 55% kwa kuwa hapo awali Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ilikuwa haito fedha zilizotegwa kwenye bajeti kwa ajili ya shughuli za lishe ila kwa sasa utekelezaji ni mzuri kwani Halmashauri inatoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa afua za lishe.
Ndugu. Asiatu Mmbwambo ni Afisa Lishe Wilaya na hapa anasema kuwa " kwa sasa utekelezaji wa shughuli za afua za lishe umepanda toka 27% hadi 55% kutokana na Halmasahauri kuunga mkono shughuli za lishe kwa kutoa fedha zilizotengwa kwenye bajeti japo sio zote. Vile vile kama Wilaya tumepanda toka katika alama nyekundu mpaka kufikia alama ya njano, hii ina maana tumetoka katika hali ya hatari na kufikia hali nzuri, lakini hali nzuri zaidi ni kupata alama ya kijani ambapo tumejipanga kuifikia alama hiyo".
Afissa Lishe wa Wilaya Ndugu. Asiatu Mmbwambo akiwasilisha mada za lishe kwa Wajumbe wa kamati ya Lishe ya Wilaya katika Kikao cha Robo ya Tatu mwaka 2019/2020 katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya.
Katika salam toka Serikali Kuu uliowasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amesema kuwa "Lishe bora ni msingi wa afya bora, hivyo lishe humjenga binadamu kimili na kiakili. Serkali katika kuchangia utekelezaji wa shughuli za lishe katika Wilaya yetu imefanya yafuatayo:Mwezi Januari 2020 imeleta tani 100 za mahindi kwa ajili ya kukizi uhaba wa chakula uliokuwepo kipindi hicho, kuwalipa mishahara watumishi wa halmasahauri wanaotekeleza shughuli za lishe ambapo kama wangeajiriwa watu binafsi kungekuwa na gharama kubwa za kutekeleza shughuli hizi na kuanzisha program ya kufanya mazoezi kila jumamosi kwa lengo la kuwajengea wananchi afya njema".
Vile vile Mkuu wa Wilaya ameshauri kuanzishwe mashamba darasa maeneo ya vituo vya kutolea huduma ya afya, shuleni, sokoni na ofisi za vijiji ili wananchi wapate ujuzi wa kuandaa mashamba na bustani kwa ajili ya vyakula vyenye virutubishi muhimu kwa afya na ukuaji wa binadamu hususani watoto. Pia ameonya kwa upande wa shule za msingi na sekondari kutunza bustani za mboga au kupanda miti isiwe adhabu kwa wanafunzi ila iwe ni shughuli za kawaida ili watoto baada ya kumaliza masomo waweze kutekeleza wakiwa nyumbani.
Pia Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa wananchi kijikinga na janga la ugonjwa wa corona kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya. Ameongeza kuwa katika Wilaya ya Mpwapwa tuna watu 21 wapo karantini kwa ajili ya ufuatiliaji.
Wajumbe wa kamati ya Lishe ya Wilaya wakifuatilia uwasilishwaji wa afua za lishe katika Kikao cha Robo ya Tatu mwaka 2019/2020 katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya.
(kulia ni Afisa Afya wa Wilaya Ndugu. Merry Mabangwa)
Kwa Maelezo na taarifa za Kina Pakua Nyaraka hizi hapa chini:
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.