Mkurugenzi Mtendajibwa Halmshauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi H Ally Novemba 18,2025 ametembelea Miradi ya kimaendeleo inayoendelea kujengwa katika Idara ya Elimu ya awali na Msingi.
Katika ziara yake hiyo amekagua ujenzi wa Mradi wa Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Ofisi 1 Shule ya Msingi Kibakwe ikiwa
Shule ilipokea kiasi cha shilingi 27,047,925/= fedha za BOOST kwa ajili ya umaliziaji.
Pia ametembelea Shule ya msingi Ikuyu iliyopokea fedha ya BOOST kwenye kifungu cha P4R kiasi cha shilingi 140,400,000/= kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, hadi sasa imetumika fedha kiasi cha shilingi 36,514,500/= kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi. Miradi ya ujenzi inayotekelezwa ni kama ifuatavyo;
Vyumba 3 vya madarasa Elimu msingi
Vyumba 2 vya Madarasa Elimu awali
Vyoo matundu 4 Elimu msingi
Vyoo matundu 6 Elimu awali
Halikadhalika, amekagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Massa iliyopokea fedha kutoka TAMISEMI kiasi cha shilingi 302,200,000/= kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Elimu ya awali na Msingi kwa kuzingatia shughuli zifuatazo;
Ujenzi wa vyumba 6 vya Madarasa Msingi
Matundu 12 ya Vyoo
Vyuma 2 vya madarasa ya awali na matundu 6 ya vyoo
Jengo la Utawala na Kichomea taka.
Wakati wa ziara yake hiyo,Mkurugenzi Mtendaji amezitaka kamati na wasimamizi wa miradi hiyo kuengeza kasi ya utendaji kazi ili kwenda sambamba na muda uliowekwa wa kumalizia mradi huo.













Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.