Maadhimisho wa wiki la lishe kitaifa yameadhimishwa Leo Novemba 21,ambapo kwa Wilaya ya Mpwapwa yameeadhimishwa katika Kata ya Berege kijiji cha Berege na kudhuriwa na Wananchi wa kila rika.
Wakati wa Maadhimisho hayo,Afsa Lishe Wilaya Ndg Eliwaza Ndau ametoa Elimu inayohusiana na makundi yote sita ya vyakula ili kuweza kupata lishe bora kwa mtoto,mama,baba na kila rika.
Pia amesisita jamii isiache kujitahidi kula vyakula vya lishe kwa kumaanisha kila penye kundi la vyakula inapaswa ule japo kidogo kidogo kwa kila siku ili uweze kukamisha mlo bora wa Lishe.
"Hakkkisheni kwa kila siku tujitahidi kula vyakula vya makundi yote sita niliyoyaelezea hata kwa kidogo kidogo tu"
Nae Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mima Ndg Irene ambae ndie mgeni rasmi wa maadhimisho hayoakimuwakilisha Mkuu wa Wilaya amesema lishe ni kwa ajili ya wote na sio kwa watu maalum.
Halikadhali ametoa rai kwa wanajamii wote wanapaswa kuyaishi kwa makundi yote sita ya vyakula ili tuweze kupata afya bora.
"Sisi kama jamiii inatupasa tuyaaishi makundi yote ya chakula ambayo yatajumuisha lishe bora"
Hata hivyo ameelezea Lengo la kauli mbiu ya lishe ni kupunguza watoto wenye utapia mlo pamoja na watu wazima, vijana ili kuweza kuepukana na udumavu wa kukosa Lishe bora.
Vilevile, amewasisitiza viongozi wote waende kuwa mabalozi kwa wenzao na pia wakawajibike katika namna ya kuiishi na lishe bora.
Maadhimsho haya yameadhimishwa na kauli mbiu isemayo "Afya ni Mtaji,Zingalia Unachokula"











Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.