Mama Samia Suluhu Hassani,ndie anaetoa fedha kujenga vituo vya afya,madaraja,Shule na zahanati.
Hayo yamebainishwa leo Disemba 02,2025 na Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Mhe George N.Malima wakati akikabidhi gari la kubebea wagonjwa (AMBULENCE)katika kituo cha Afya Matomondo.
Akizungumza wakati wa kutoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa Matomondo kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema Mama Samia ndie anaetoa magari haya ya kubebea wagonjwa,ndie anaetoa fedha za kujengea vituoa vyaafya,madaraja,shule pamoja na zahanati sisi ni wawakilishi wake tu,amabe tunapeleka shida za jimboni na kuweza kuzitatua.
Pia amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi Mwanahamisi H Ally kwa kuwa bega kwa bega katika usimamizi mzuri wa fedha zinazoletwa kutoka Serikali kuu za miradi bila kuzifanyia Uchakachuzi wowote.
Nae,Mganga Mkuu Wilaya Dr Stanley Mlay ameelezea mafanikio ya utoaji wa huduma za afya ikiwemo ongezeko la vituo vya afya na zahanati pamoja na vyombo vya usafiri kwa sababu husaidia kufika kwa urahisi maeneo ambayo yalikuwa hayafikiki kiurahisi,pia hurahisisha katika kuokoa maisha ya wamama wajawazito na wagonjwa wengine.
Hata hivyo,Afisa Mipango Wilaya Ndg Dismas Pesambili ambae ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji amesisitiza Utunzaji wa gari hilo la kubebea wagonjwa (AMBULENCE) na kuwaasa lisipotunzwa watarejea kulekule walipotoka,na kusisitiza kutumika katika kazi za kituoni hapo tu na si kwa shuhuli binafsi na ikigundulika hivyo hatovumiliwa mtu yoyote kwa kitendo hicho.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika kituo cha Afya Matomondo yakihudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Richard Maponda,Makamo Mwenyekiti Mhe Baraka Habari,Diwani wa kata ya Matomondo,wa Kata ya Mlembule na Diwani wa kata ya Kimagai pamoja na viongozi tofauti wa dini,wa Chama na Wananchi mbali mbali wa kata ya Matomondo.






Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.