Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wamepewa mafunzo ya namna ya Uendeshaji wa Shuhuli za Serikali za Mitaa leo Januari 29,2025.
Mafunzo hayo yametolewa katika kata ya Ipera,Mang'aliza,Galigali na Malolo yakiwa na Lengo la kuwapa uwezo Viongozi hao katika utekelezaji wao wa majukumu ya Kiuongozi.
Halikadhalika Afisa Utawala Bora Wilaya Bw.Thomasi Magari ameelezea muundo wa kamati za Halmashauri ya Kijiji na majukumu yake pamoja na kazi ya kila Kamati na kutoa msisitizo kwa viongozi kuzingatia kuitisha kwa mikutano ya kila robo ili iweze kusaidia utoaji ŵa maamuzi wakati wanapofanya Mkutano mkuu.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.