Mradi wa Pamoja Tuwalishe ni mradi unaojikita na utoaji wa Chakula kwa elimu,Januari 31,2025 umefanya kikao cha kupanga ratiba ya kuhamasisha wazazi,walezi na jamii ya Wilaya ya Mpwapwa katika Ukumbi wa Halmshauri ikiwa na lengo la Utambulisho wa Mpango wa Twaweza na kupanga ratiba ya mikutano ya uhamasishaji.
Wakati wa kikao hicho Mratibu wa Mpango wa Twaweza Bw.Hillay Darushina amesema mpango wa twaweza unatekelezwa katika vipengele saba ambapo vipenegele sita ni kwa ajili ya kuinua taaluma ya Msingi Shuleni na kimoja kwa ajili ya jamii ambayo itaendeleza kuinua taaluma hiyo.
Halikadhalika ameelezea mpango wa twaweza ni kutekeleza kwa kutumia mfumo wa vikundi vidogo vya huduma za kifedha na kutumia njia za kuhamasisha wazazi,walezi na jamii kwa lengo la kumnufaisha mtoto anaesoma shule zinazonufaika na mradi huo wa Pamoja Tuwalishe.
Vilevile amefafanua lengo la utekelezaji wa mradi ni kuwainua wazazi kiuchumi,hali ya usalama wa chakula pamoja na ushiriki wa wazazi,walezi na jamii katika utekelezaji wa moja kwa moja wa mradi.
"Mradi utahamasisha wazazi,walezi na jamii na vikundi vya mradi vitaitwa Vikundi vya Twaweza vya Mradi wa Pamoja Tuwalishe"
"Lengo la utekelezaji wa mradi ni kuinua wazazi kiuchumi kwa manufaa ya kuweza kuweka na kukopa lakini pia kupata mafunzo ya kilimo ili kuinua usalama wa chakula Shuleni" Amesema Darushina
Nae muwakilishi kutoka Mkoani Bi.Rustika Turuka ametoa shukrani kwa wanamradi na kuwataka watendaji kusimamia kazi zao vizuri na kuwasisitiza walimu kutimiza wajibu wao wa kuwafundisha ili kuweza kupata matokeo mazuri.
"Elimu,afya,kilimo watendaji mnapaswa kusimamia kwenye mambo yote haya"
Akizungumza mmoja wa wanufaika wa mradi wa Pamoja Tuwalishe amewashukuru kwa kuengezeka ufaulu mzuri Shuleni,wanafunzi kuacha utoro pamoja na kupanda kitaaluma hali àmbayo hapo mwanzoni haikuwepo.
"Shukrani kwa hali nzuri Shuleni kwa kupandisha ufaulu,wanafunzi kuacha utoro na hata kuinuka kitaaluma"
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.