Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wameendelea kupata mafunzo ya namna ya uendeshaji wa shuhuli za Serikali za Mitaa leo Febuari 04,2025 katika Kata ya Mima,Berege,Iwondo na Chitemo.
Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwapa uwezo Viongozi hao katika utekelezaji wao wa majukumu ya Kiuongozi katika Kata zao.
Halikadhalika Afisa Utawala Bora Wilaya Bw.Thomasi Magari ameelezea muundo wa kamati za Halmashauri ya Kijiji na majukumu yake pamoja na kazi ya kila Kamati na kutoa msisitizo kwa viongozi kuzingatia kuitisha kwa mikutano ya kila robo ili iweze kusaidia utoaji ŵa maamuzi wakati wanapofanya Mkutano mkuu.
Hata hivyo Bw.Magari amewataka Viongozi wa Vijiji na Vitongoji wawe wanashirikiana katika upangaji wao ili waweze kufanikisha usimamizi mzuri wa mipango ya miradi, kutambua takwimu sahihi za vijiji na vitongoji vyao pamoja na kujikita zaidi katika uanzilishi wa Miradi ya kimaendeleo.
Nae Mwanasheria wa Wilaya Bi Martina amewafafanua sheria mbali mbali ndogo ambazo wanaweza kuzitumia kama vyanzo vya kuingizia mapato katika vijiji vyao huku akiwataka pindi wanapozitunga sheria hizo zinapitishwa katika Mkutano mkuu na kuzileta wilayani ili ziweze kupitiwa na mwanasheria,na mwisho kupitishwa kwenye baraza la Madiwani.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.