Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene ameonya matumizi ya gari ya wagonjwa (ambulance) iliyotolewa na Serikali katika Kituo cha Afya cha Mtera lisitumike kubeba magendo badala yake itumike kwa ajili ya malengo yaliyokusudiwa
Waziri Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Jumanne Januari 7, 2024
wakati wa hafla ya kukabidhi gari hiyo mara baada ya kufanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Mtera , Kibakwe iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma ambapo amesema gari hiyo ni mali ya Serikali
" Msisitizo wangu gari hii ni ya wagonjwa ni mali ya Serikali muitumie kurahisisha utoaji huduma bora kwa wananchi na sio vinginevyo , Nataka kuona gari hii inatumiwa na watanzania wote ’ amesisitiza Mhe.Simbachawene
Amefafanua kuwa azma ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa gari hiyo ni kuhakikisha inasaidia kuwafikisha wagonjwa katika hospitali ya Rufaa kwa muda muafaka pale ambapo mgonjwa amepewa rufaa ya matibabu hususan akina Mama wajawazito.
‘‘ Tunataka tukiliona gari hili likiwa linatembea barabarani liwe limebeba mgonjwa au linaenda kumfuata mgonjwa’’ amesisitiza Mhe. Simbachawene
Amesema ujio wa gari hiyo katika kituo hicho ni mageuzi makubwa yanayofanywa na Serikali ambapo zaidi ya wananchi 14,000 katika Kata ya Mtera wanatarajiwa kunufaika kupitia gari hiyo.
Katika hatua nyingine, Mhe. Simbachawene amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuhakikisha dereva atakayekuwa akiendesha gari hilo atoke karibu na Kituo hicho cha Afya ili gari hilo liweze kutoa huduma kwa wagonjwa mara tu pale dharula inapojitokeza
Aidha, Mhe.Simbachawene ametoa wito kwa akina mama wajawazito kuwahi katika vituo vya afya mara waonapo dalili za kuanza kwa uchungu ili kuepuka vifo visivyo vya lazima huku akiwasihi manesi kuwahudumia wagonjwa kwa upendo kama viapo vyao vinavyowataka
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.