Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Selemani Said Jafo amefanya ziara Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma kwa kutembelea na kukagua miradi ya Barabara, Kituo cha Afya na Miradi ya Maji.
Katika ziara hiyo Mh. waziri amekagua barabara ya lami ya Mpwapwa mjini yenye umbali wa kilometa moja, kuanzia Ujenzi (Round About) hadi Mtaa wa Hazina. Alipatiwa maelezo mafupi juu ya barabara hiyo na amempongeza maneja wa TARURA Eng. Geofrey Mkinga kwa usimamizi mzuri wa barabara hiyo iliyogharimu Shilingi za kitanzania Milioni Mia tato na tato (Tsh. 505,000,000.00). Akiwa anaendelea kukagua barabara hiyo alijionea korongo kumbwa linalopita katikati ya Mpwapwa Mjini amablo wakati wa masika husababisha mafuriko na maafa kwa wakazi wa Wilaya ya Mpwapwa. Pamoja na kuelezwa mikakati ya kulidhibiti korongo hilo aliita Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Wataalamu wengine watoe mikakati dhabiti ya kulidhibiti korongo hilo kwa kuwa lipo katika sura ya mji wa Mpwapwa.
Mh. Waziri Jafo akikagua barabara ya lami ya Mpwapwa mjini.
Mh. Waziri Jafo akikagua barabara ya lami ya Mpwapwa mjini.
Mh. Waziri Jafo akitoa maagizo ya namna ya kuthibiti korongo lililopo katikati ya Mpwapwa mjini.
Aidha waziri huyo wa OR TAMISEMI ametembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha Afya cha Mima kinachojengwa na Mkandarasi Global Space East Africa kwa kutumia teknolojia ya PRE-FABRICATED MATERIALS ni ya kisasa na mpya kwa Taifa la Tanzania. Ujenzi huo utatumia Tsh. 500,000,000.00 hadi kukamilika kwake, ambapo majengo yanayojengwa ni Jengo la Upasuaji- thamani yake ni Tsh. 153,520,151/=, Nyumba ya mtumishi - thamani yake ni Tsh. 90,094,822/=, maabara- thamani yake ni Tsh. 140,314,975/=, wodi ya watoto- thamani yake ni Tsh. 53,933,581/=, na wodi ya kina mama - thamani yake ni Tsh. 62,136,122/=. Vile vile majengo mengine yaliyopo katika mkataba na yatajengwa ni kichomea taka na jengo la kuhifadhi maiti. Kwa sasa majengo matano ujenzi wake umeshaanza ambayo ni jengo la upasuaji, nyumba ya mtumishi, maabara, wodi ya watoto na wodi ya kina mama.
Pamoja na kukagua mradi huo wa kituo cha Afya Mh. Jafo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kufanikisha kufika hatua ya kujenga kituo cha Afya cha kisasa kwa kuwashirikisha wananchi katika hatua zote za ujenzi wa mradi huo.
Pia Mh waziri ameagiza ifikapo tarehe 15 Februari 2018 mradi huo wa Kituo cha Afya Mima uwe umekamilika. Sambamba na hilo waziri Jafo amewaagiza wakurugenzi nchi nzima kuwapelaka madaktari kusomea taaluma ya USINGIZI kwa kozi za muda mfupi na mrefu ili waweze kutoa huduma pindi mgonjwa anapokuwa anahitaji kufanyiwa upasuaji na baada ya kufanyiwa upasuaji. Agizo hilo limekuja kutoka na ukweli kwamba vituo vyote vya afya nchini vitatoa huduma ya upasuaji na wataalamu wa usingizi ni wachache.
Mh. Waziri Jafo akipata maelezo ya mradi wa kituo cha Afya cha kisasa Mima toka kwa Mkandalasi wa kampuni ya Global Space East Africa .
Mh. Waziri Jafo akikagua moja ya jengo ambalo limetumia teknolojia ya Pre-Fabicated materials katika kituo cha Afya Mima
Mh. Waziri Jafo akishiriki katika ujenzi wa kituo cha Afya Mima kwa kuunganisha chuma kinachoshirikilia msingi (zege) na ukuta (pre-fablicated materials).
Mh. Waziri Jafo akishiriki katika ujenzi wa kituo cha Afya Mima kwa kukata moja ya kifaa cha chuma kitakachotumika katika ujenzi huo.
Aidha Mh. waziri ametembelea na kukagua miradi miradi ya maji katika kata ya Mima yenye thamani ya fedha za kitanzania Tshs 428,929,937.00 na unatekelezwa kwa ufadhili wa WSP kupitia program ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (NRWSSP) na kumuagiza Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Mpwapwa, Eng. Msengi kuhakikisha ujenzi wa vituo vya maji (DPs ) unakamilika kwa wakati na kutoa maji ya kutosha kwa mahitaji ya wananchi. Vile vile amemuagiza mhandisi huyo kuhakikisha mamboma ya maji yanayotumika yawe yamekidhi vigezo na viwango ili yasiweze kupasuka kutokana na msukumo wa maji.
Mh. waziri akikagua miradi ya maji kata ya Mima na kutoa maelekezo kwa Mhandisi wa maji.
KWA TAARIFA ZAIDI PAKUA TAARIFA ZIFUATAZO............
TAARIFA YA MRADI WA KITUO CHA AFYA MIMA.pdf
TAARIFA YA UJENZI KITUO CHA AFYA MIMA.pdf
TAARIFA YA WILAYA YA MPWAPWA KWA ZIARA YA MH. WAZIRI JAFO.pdf
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.