Siku ya Familia Duniani huadhimishwa kila mwaka Mei 15, na Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. Maadhimisho hayo yanatokana na Tamko la Baraza la Umoja wa Mataifa Na. 47/257 la tarehe 20 Septemba 1993 lililoidhinisha siku maalum kwa ajili ya familia.
Tanzania ni moja ya Nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa, hivyo huungana na nchi zingine kila mwaka kuadhimisha siku hii. Mwaka huu maadhimisho yanafanyika kiwilaya kwa kuzingatia utaratibu watakao jiwekea na ma mazingira ya Wilaya husika.
Kwa willaya ya Mpwapwa maadhimisho hayo yamefanyika kwa kuanza na kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ambapo wananchi na wadau mbalimbali wamehudhuria katika kufanya usafi. Pia maadhimisho hayo yameenda sambamba na Uzinduzi wa Vitambulisho vya Matibabu Bure kwa Wazee.
Mgeni rasmi katika Maadhibisho hayo ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime, ametoa hotuba fupi yenye maudhui ya kuhamasisha, kuhimiza, kuelimisha na kuitanabaisha jamii kuhusu umuhimu wa familia na malezi bora kwa watoto ili kupata kizazi cha watoto wenye maadili mema katika jamii.
Mhe. George Fuime (Makamu Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Mpwapwa) akihutubia wananchi katika maadhimisho ya siku ya familia
Aidha Mgeni rasmi amefafanua Kauli mbiu katika ya mwaka 2018 kuwa ni "Malezi Jumuishi ni Msingi wa Uzalendo, Utu na Maadili ya Familia na Taifa" ambayo inalenga kuhamasisha familia umuhimu wa malezi kwa watoto na kutenga muda wa kukaanao kwa pamoja ili kujiepusha na matukio ya ukatili dhidi ya watoto na kuelimisha jamii kuachana na mila na desturi zenye kuleta madhara pamoja na imani za kishirikiana.
Pia amewakumbusha wanafamilia kutimiza wajibu wao katika upatikanaji wa Elimu na Malezi bora kwa watoto .
Vilevile Mgeni rasmi amezindua viambulisho vya matibabu bure kwa wazee ambapo wazee 170 wa kata ya Mpwapwa mjini wamepatiwa vitambulisho vyao. Aidha amesema zoezi hili la vitambulisho ni endelevu na kwa kuanza tumeanza na kata ya Mpwapwa Mjini na litaendelea katika kata zote za Wilaya ya Mpwapwa.
Mgeni rasmi (wa pili toka kulia ) akikabidhi kitambulisho cha matibabu bure kwa mzee.
Mzee akitoa neno la shukrani kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa kwa kuwaona wazee ni azina muhimu na kuwawezesha kupata matibabu bure.
Wazee wakisubiri kupatiwa vitambulisho vyao vya matibabu bure
Baadhi ya vitambulisho vilivyotolewa kwa wazee
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.