Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya Ndg:Obert Mwalyego wakati wa Maadhimisho ya Wiki la unyonyeshaji Duniani,apambo kiwilaya ilifanyika katika Kanisa la KKT Mpwapwa Agosti 7,2024.
Ndugu Mwalyego amewataka kina mama wazingatie siku elfu moja za makuuzi ya mtoto tangia mimba inapotunga hadi kufikisha kwa umri wa miaka miwili kwa mtoto,na kuwasisitiza kina mama kipindi cha ujauzito wapate lishe bora kwa lengo la kumkinga mtoto na kuweza kupata makuuzi mazuri.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya ya Mpwapwa Dkt Bonifasi Hassan amesema siku hii inaadhimishwa kwa faida mbalimbali zinazopatikana katika maziwa ya mama kama vile kumpatia virutubisho vyote vya uwiano sahihi pamoja na kumpatia kinga katika mwili wake ya kupata magonjwa,pia humkinga mama na kaupata ujauzito kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya unyonyeshaji.
Hata hivyo amesema maziwa ya mama ndio stahiki kutokana na kuwa na joto sahihi na kuweza kukata kiu bila ata kupewa maji.
Kauli mbiu ya mwaka huu isemayo "Tatua changamoto,saidia unyonyeshaji wa watoto" inalengo la kuziba pengo la asilimia zilizobaki za unyonyeshaji.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.