Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wametakiwa kufanya kazi kwa Weledi,Juhudi na Maarifa kwa kuzingatia Sheria,Kanuni na Taratibu pamoja na miongozo yote,hayo yamebainishwa leo Septemba 15,2025 katika Ukumbi wa Shule ya Mpwapwa Sekondari na Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Dodoma Dkt Khatib Kazungu.
Wito huo umetolewa leo wakati wa kikao cha kuzungumza na Watumishi mbali mbali kutoka Taasisi na Kada tofauti mara baada ya kufika kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na Watumishi hao.
"Tuendelee kufanya kazi kwa Weledi,Juhudi,na Maarifa kwa tukizingatia Sheria,Kanuni na Taratibu pamoja Miongozo yote ambayo imetungwa na Viongozi wetu"Amesema Dkt kazungu.
Halikadhalika amesisitiza kufanya kazi kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050,kuzingatia malengo ya Mileniam, kuzingatia Ilani ya Chama,na kuzingatia Mpango mkakati wa Halmshauri ya Mpwapwa.
Kabla ya Kuteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt Kazungu amewahi shika nyadhifa mbalimbali Serikalini ikiwemo Naibu katibu Mkuu Wizara ya Nishati.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.