Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime amefungua Mafunzo ya Siku mbili kuanzia leo tarehe 11/08/2018 hadi 12/08/2018 kwa watu wenye ulemavu ambayo yamefanyika katika Ukumbi Mkubwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Katika ufunguzi wa mafunzo haya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa amewatambulisha waliohudhuria katika mafunzo haya ni pamoja na watu wenye walemavu, baadhi ya wakuu wa idara, watendaji wa kata na vijiji, baadhi ya waheshimiwa madiwani, afisa ustawi mkoa, mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu mkoa wa Dodoma na mkufunzi toka Chama cha Watu wenye ulemavu taifa ambaye pia ni wakili wa watu wenye ulemavu.
Pia Makamu Mwenyekiti ameeleza madhumini ya mafunzo haya ni kuendelea na mradi wa kutoa utetezi kwa watu wenye ulemavu ili waweze kushiki katika nyanja mbalimbali ikwepo kiuchumi, kijamii, kisiasa na kujali na kuheshimu utu wao. Mradi huu na mafunzo haya yanafadhiliwa na shirika la FCS (Foundation for Civil Society) na unatekelezwa na Chama cha Wasiona Mkoa wa Dodoma, na uliaza kutekelezwa katika Wilaya ya Chamwino na Mpwapwa kwa kata nne tu kila wilaya ambapo mpaka sasa mradi huu una muda wa miaka miwili. Kwa upande wa Wilaya ya Mpwapwa mradi huu wa Utetezi wa watu wenye ulemavu unatekelezwa katika kata ya Kimagai, Mpwapwa Mjini, Godegode na Vinghawe.
Washiriki wakiwa katika mafunzo ya watu wenye ulemavu katika Ukumbi wa Mkubwa wa Mikutano Wilayani Mpwapwa (Picha Na: Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA Mpwapwa)
Akizungumza malengo ya mradi huu Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Dodoma kuwa ni kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli mbalimbali, kuwa na bajeti jumuishi katika Halmashauri yetu, kuwajumuisha watu wenye ulemavu katika mipango ya maendeleo, kuona kamati za watu wenye ulemavu zinaundwa na zinafanyakazi, na kutoa mafunzo kama haya ya leo ili kuwajengea uwezo na uelewa kwa watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu ili wote kwa pamoja waweze kufahamu mahitaji ya watu wenye ulemavu.
Mmoja wa Washiriki akichangia mada katika mafunzo ya watu wenye ulemavu katika Ukumbi wa Mkubwa wa Mikutano Wilayani Mpwapwa (Picha Na: Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA Mpwapwa)
Mfunzo ya leo yanafanyika kwa ajili ya kuwaelimisha watu wenye ulemavu na watu wasio na ulemavu ili wote kwa pamoja waweze Kuifahamu na kuitekeleza sheria ya watu wenye ulemavu namba 9 ya mwaka 2010.
Akitoa mafunzo hayo mwezeshaji wa mafunzo Ndug. Novath Rukwago ambaye pia ni mwanasheri wa Chama cha Walemavu Taifa, ameitambulisha sheria ya watu wenye ulemavu na utekelezaji wake. Amefafanua kuwa lengo la mafunzo hya ni kuwawezesha watu wenye ulemavu na viongozi wa Wilaya kuifahamu na kuitekeleza sheria ya watu wenye ulemavu namba 9 ya mwaka 2010.
Pia ameeleza kuwa Serikali imeamua kutunga sheria hii ni kwa kuwa inawathamini na kujali utu wa watu wenye ulemavu na hivyo kupitia sheria hii watu wenye ulemavu wanatakiwa kushirikishwa katika kuandaa vipaumbele vyao, mipango na bajeti, kuwewesha kupata fedha ya iliyotengwa katika bajeti ya Halmashuri ya Wilaya ya 2% ya bajeti yote iili watu wenye ulemavu waweze kutekeleza mahitaji yao. Vile vile haitaruhusiwa fedha za watu wenye ulemavu kubadilishwa matumizi au kutowapatia kwa kusingizio cha bajeti kuwa finyu. Sheria iko wazi kwa yeyote atakayeivunja sheria hii atapata adhamu.
Mwezeshaji ametoa wito kwa watu wasio na ulemavu kuto wanyanyapaa watu wenye ulemavu kwakuwa hata wao ni walemavu watarajiwa, kuwa kuwa ulemavu unaweza kuupata kwa ajali, kuuguwa muda mrefu, kuzaliwa, na kuwa na umri mkubwa.
Mwezeshaji Ndug. Novath Rukwago (mbele) akitoa mafunzo ya watu wenye ulemavu katika Ukumbi wa Mkubwa wa Mikutano Wilayani Mpwapwa (Picha Na: Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA Mpwapwa)
Washiriki wakiwa katika makundi matatu wakijadili maswali waliyopewa na mwezeshaji wa mafunzo ya watu wenye ulemavu nje ya Ukumbi wa Mkubwa wa Mikutano Wilayani Mpwapwa (Picha Na: Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA Mpwapwa)
Katika kufunga mafunzo haya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime ameelezea kwa mifano FURSA wanazopatiwa walemavu katika Wilaya ya Mpwapwa ni pamoja na kushirikishwa katika vikao, ajira, kushiriki shughuli za uchumi na siasa. Akitolea mfano wa watu wenye ulemavu na wameshirikishwa katika nyanja mbalimbali kwa kujali utu wao ni pamoja na Afisa Mtendaji wa Mpwapwa Mjini ambaye ana ulemavu wa ngozi na kwa sababu hiyo amepangwa mjini na yupo katika ajira ya kudumu, mwingine ni Fundi Mkuu wa Idara ya Ujenzi Ndug. Kandido ambaye anaulemavu wa miguu na ameajiliwa kama fundi wa magari na vyombo vya moto mkatika idara ya ujenzi, ila pasipo kumbagua amepewa cheo cha kuwa fundi mkuu hata kama ni mlemavu.
Vile vile Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ameongeza kuwa, yupo mwenyekiti wa Mtaa katika kijiji cha Ilolo ni mlemavu wa macho na amechaguliwa na wanachi bila kujali kuwa yeye ni mlemavu wa macho.
Haya ni mambo machache tu ambayo yanaonyesha kuwa walemavu wilayani mpwapwa wanapatiwa fursa katika kujikwamua kimaisha na kushirikishwa katika mambo ya maendeleo ya taifa letu.
Mkamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime (aliyesimama) akichangia mada katika mafunzo ya watu wenye ulemavu katika Ukumbi wa Mkubwa wa Mikutano Wilayani Mpwapwa (Picha Na: Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA Mpwapwa)
Kwa taarifa kwa kina pakua nyaraka hii:
Mafunzo kwa Watu Wenye Ulemavu yaliyofanyika Wilaya ya Mpwapwa.pdf
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.