(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imeadhimisha Siku ya Mtoto Afrika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chazungwa ambapo watoto toka katika Shule za Msingi na Sekondari wamehudhuria. Sherehe hizo zimehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa idara, taasisi, waheshimiwa madiwani pamoja na watoto toka Compasion katika Kanisa la KKKT Mpwapwa.
Katika Sherehe hizo Mgeni rasmi ni Mhe. Honorati Pima ambaye ni diwani wa kata ya Kingiti ambaye pia amemwakilisha Mhe. George Fuime Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa na Diwani wa Kata ya Mpwapwa Mjini aliyetakiwa kuwa mgeni rami na alishindwa kuhudhuria kutokana na majukumu mengine ya kikazi.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii na Vijana Ndug. Patric Mafuru akitoa msaada wa sabuni na sukari kwa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa Wodi namba 7
Katika Hotuba yake mgeni rasmi amesema kuwa "Watoto wanahaki ya kupendwa, kulindwa na kupewa msaada pale unahitajika kwa sababu watoto ni miongoni mwa makundi yenye mahitaji maalum hivyo jamii tuna wajibu wa kuwasaidia na kutoa taarifa kwa wenye uhitaji ili waweze kusaidiwa".
Katika kuadhimisha sherehe hizo Mgeni rasmi amepata fursa ya kuongea na watoto wenye ulemavu wa akili wanaosoma katika Shule ya Msingi Chazungwa pamoja na kuwapatia zawadi za sabuni na sukari takribani watoto 50 wakiwa na wazazi wao.
Vile vile mgeni rasmi na wageni waalikwa wamepata fursa ya kutembelea wodi ya watoto katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa na kuwagawia sukari na sabuni kawa watoto zaidi ya 20 waliolazwa hospitalini hapo wakiwa wanaendelea katika matibabu.
Aidha wazazi wa watoto waliopatiwa msaada huo wameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa pamoja na wadau wote waliofanikisha kupatikana kwa msaada huo. Pia wametoa wito kwa jamii kuwa na moyo wa kuisadia jamii yenye mahitaji maalum.
Mgeni rasmi Mhe. Honorati Pima (wa kwanza kulia) alitoa msaada wa sabuni na sukari kwa watoto wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Chazungwa
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.