Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndg Dismas Pesambili ameongoza kikao cha Makisio ya ukusanyaji wa mapato wa mwaka wa fedha 2025/2026 na kuwataka kuandaa mikakati madhubuti ya ukusanyi wa mapato ili kuweza kufikia kiwango cha makisio cha mwaka wa fedha 2025/2026
Hayo yamebainishwa leo Septemba 23,2025 wakati akizungumza na Watendaji kata wa kata zote 33 za Wilaya ya Mpwapwa kwa lengo la kutoa maelekezo na mikakati ya kuweza kufikia lengo.
"Tunatakiwa kuandaa mikakati madhubuti ambayo itatusaidia katika ukusanyi wetu wa mapato na kuweza kufikia kiwango cha makisio" Amesema Pesambili
Halikadhalika, Watendaji Kata hao wameweza kuchangia na kutoa changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili na kukutana nazo wakati wa ukusanyaji wa mapato hayo ikiwemo uhaba wa mazao kwa wakulima,uhaba wa vitendea kazi na kutokuwepo kwa Usafiri kwa maeneo ya mbali.
Hata hivyo wametoa mapendekezo ambayo yatasaidia kutatua baadhi ya changamoto wanazokutana nazo ikiwemo kuongezewa posi za kukusanyia mapato pamoja na kupatiwa usafiri kwa kila Mtendaji kata wa maeneo ya mbali.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa mwaka wa Fedha wa 2025/2026 inamakisio ya ukusanyaji wa mapato Shilingi Billion 3,710,136,000.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.