Wataalam hao waliokutembelea Kituo Kimoja cha Biashara (One Stop Business Center) ni Afisa Biashara, Afisa TEHAMA, Mhandisi na Mhasibu wa Mapato. Wataalam hao walielezwa kimamilifu jinsi kituo hicho kinavyofanyakazi na kuweza kutoa leseni ya biashara na vileo ndani ya siku moja.
Katika kituo hicho Kuna Ofisi ya Benki ya NMB, Mfamasia, Afisa Maliasili, Afya, Ardhi, Mhasibu na Mtendaji wa Baraza la Biashara la Wilaya. Vile vile kuna ukumbi wa mikutano na kituo chote kimefungwa Miundombinu Kiwambo ya Kompyuta (Local Area Network).
Maafisa wote wa ofisi hizo wapo katika kituo hicho na wanaendelea na majukumu yao ya kila siku isipokuwa Benki ya NMB ambao wanakamilisha hatua za mwisho za kuhamia hapo.
Pia katika kituo hicho kuna mifumo mikuu mitatu inafanya kazi kila siku kama ifuatavyo:-
1. Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji Mapato (LGRCIS).
2. Mfumo wa BRELA: kwa ajili ya kusajili majina ya biashara za wateja.
3. Mfumo wa Benki ya NMB unaoitwa Cash Collection System (CCS)
Aidha walielezwa changamoto kubwa ya kituo hicho katika kuhakikisha inatoa leseni ndani ya siku moja ni ukosefu wa TIN namba kwa wafanyabiashara ambao wanatakiwa kwenda Dodoma Mjini kufuata TIN namba hizo. Pia Afisa Biashara Wilayani Mpwapwa aliwaomba wataalam hao walichukue kama changamoto kubwa katika kituo hicho na waweze kutafuta njia ya kusaidia kutatua.
Jengo la Kituo Kimoja cha Biashara (One Stop Business Center)
Jengo la Kituo Kimoja cha Biashara (One Stop Business Center)
Jengo la Kituo Kimoja cha Biashara (One Stop Business Center)
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.