Hayo yamebainishwa leo Oktoba 26 ,2025 na Msimamizi Msaidizi wa Jimbo la Mpwapwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wasimamizi wakuu na wasimamizi wa saidizi wa vituo vya kupigia kura wa vituo 304 vya Mpwapwa yatakayowawezesha kusimamia uchaguzi mkuu kwa Utii na weledi unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 oktoba 2025.
Akifungua mafunzo mara baada ya kiapo cha utii Ndugu Underson Mwamengo ambae ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na tume huru ya taifa ya uchaguzi.
"Jambo kubwa ambalo ninawasisitiza washiriki wa mafunzo haya ni kuzingatia sheria taratibu kanuni na miongozo ili uchaguzi uweze kufanyika kwa amani na utulivu", amesema Ndugu Mwamengo
Sambamba na hilo Ndugu Mwamengo amewataka wasimamizi hao kujiepusha kuwa vyanzo vya malalamiko au vurugu wakati wa mchakato wa uchaguzi, kufanya kazi kwa ushirikiano, kufika mapema kabla ya muda wa kufungua kituo kwa ajili ya maandalizi, kuwa nadhifu na kutumia lugha nzuri pamoja na kutoa kipaumbele kwa wapiga kura wenye mahitaji maalum pindi watakapofika kituoni.
Jimbo la Mpwapwa lina jumla ya vituo 304 na Jimbo la kibakwe lina jumla ya vituo 328 vya kupigia kura katika kata 33.
"KURA YAKO HAKI YAKO JITOKEZE KUPIGA KURA"






Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.