Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi (TASAF) Bw.Peter Ilomo amefanya ziara ya kukagua mradi wa Kituo cha Afya Lwihomelo kilichopo Kata ya Wotta na Wangi Machi 21,2025.
Wakati wa ziara hiyo Bw. Ilomo amekagua jengo la kuhifadhia Maiti, jengo la kufulia, jengo la mama na mtoto pamoja na la upasuaji, jengo la wagonjwa wa Nje, Nyumba 2 in 1 za watumishi pamoja na kichomea taka, yakiwa yamegharimu jumla ya Shilingi 652,177,482.37, baada ya ukaguzi huo amepata nafsi ya kuzungumza Wananchi wa Kijiji hicho cha Lwihomelo ambao ndio wanufaika wa mradi huo na baadae kutoa shukrani zao za dhati kwa kuletewa mradi katika kijiji chao.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.