Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri ametoa wito kwa wananchi wote wa wilaya ya Mpwapwa kufanya usafi katika maeneo ya makazi, biashara na ofisi. Haya yamesemwa na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ambaye ni Kaimu Katibu tawala wa Wilaya ya Mpwapwa Ndg. Apolonia Temu katika Kijiji cha Gulwe na Chiseyu kata ya Gulwe ambako wakuu wa idara na pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya walienda kuhamashisha wananchi kufanya usafi.
Kaimu katibu tawala wa wilaya ya Mpwapwa Ndg. Apolonia Temu (kushoto) akifanya usafi katika moja ya barabara ya kuelekea zahanati ya kata ya Gulwe. (Picha na Shaibu J. Masasi Afisa TEHAMA-Mpwapwa)
Usafi umefanywa katika zahanati ya Gulwe na katika eneo la Chiseyu kunakojengwa zahanati ambapo wananchi wamejitokeza kwa wingi ili kujumuika na wataalam wa halmashauri pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama katika kufanya usafi wa mazingira.
Sambamba na kufanya usafi, pia miti ya mikorosho imepandwa na viongozi wa wilaya wakiongozwa na kaimu katibu tawala huyo. Hakika uongozi wa kata umeaidi kuituza miti hiyo ya mkorosho takribani 8 na wananchi wamesema wataongeza miche zaidi ya zao hilo la korosho katika mashamba yao wanachohitaji ni ushirikiano toka idara ya kilimo ili kufanikisha azima hiyo, ambapo mwakilishi wa kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Ndg. Baraka Msuya (Afisa Maendeleo ya jamii) ameaidi kutoa ushirikiano kwa wananchi toka kupata mbege au miche, ushauri wa kitaalam na dawa za kuua wadudu zitatolewa bure kwa wale watakaopanda miche ya mikorosho.
Akieleza ujumbe wa mkuu wa wilaya kwa wananchi wa Gulwe, Ndg. Temu amesema "Mkuu wa wilaya ameagiza kuwa kila siku kila mwananchi anapaswa kufanya usafi katika makazi yake na sehemu anazofanyia biashara na isiwe jumamosi ya kila mwisho wa mwezi tu, atakayeshindwa kufanya usafi na kukabainika katika makazi yake kuwa ni machafu hatua kali zitachukuliwa dhidi yake" . Pia Temu ameongeza kuwa "Timu nzima ya wilaya imekuja hapa kwa ajili ya kuhamasisha na kuwaelimisha juu ya usafi, na sio kila siku watakuja hapa kufanya usafi". Hivyo viongozi wa kata zote za Mpwapwa muwahamasishe wananchi kujitokeza wa wingi kufanya usafi wa mazingira na wasiofanya wachukuliwe hatua.
Vile vile kaimu katibu tawala huyo amewataka wananchi wa kata ya Gulwe na Mpwapwa kwa ujumla kuchangamkia fursa zitakazopatikana kutoka na ujenzi wa reli ya treni ya mwendo kasi (Stanadrd Gauge Railway) kama vile kuwekeza katika kibiashara, kilimo, nyumba bora, nzuri na za kisasa za kulala wageni, vyakula na biashara mbalimbali kwa kuwa tunatarajia kuwa na wageni wengi sana kutoka nje na ndani ya nchi ya Tanzania kufika Mpwapwa.
Wananchi na wataalam wa halmashauri ya Mpwapwa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wakifanya usafi kata ya Gulwe (Picha na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.