Na: Shaibu J. Masasi; Afisa TEHAMA - Mpwapwa Dc
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amefungua Mafunzo Sahihi ya Ungonjwa wa Virusi vya CORONA-19 katika Ukimbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya leo hii asubuhi. Mafunzo haya yametolewa na wataalam wa Idara ya Afya wa Wilaya wakiongozwa na Mganga Mkuu wa Wilaya Dr.Archard Rwezahura. Aidha Mfunzo hayo yamehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Wakuu wa Idara wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Wakuu wa Taasisi, Wamiliki wa Nyumba za Kulala wageni, Wamiliki wa Mabasi, Wamiliki wa Malori, Wamiliki wa Hoteli, Wanunuzi na wasambazaji wa bidhaa ya vyakula. na viongozi wa dini.
Akifungua Mafunzo haya Mhe. Shekimweri amemtaka Mganga Mkuu ajikite katika maeneo ya msingi ya ungonjwa huu kama vile chanzo, unavyosambaa, dalili, tiba au chanjo, na athari zake ili kuwafanya wadau wote waweze kuelewa kwa urahisi. Ameongeza kuwa wakati mwingine ukiongea historia, na mambo mengi ya kitaalam yanaweza yasieleweke vizuri na hivyo kila mmoja atashindwa kuwa balozi katika kufikisha ujumbe huu wa wengine. Vilevile Mkuu wa Wilaya amewasisitiza wadau waliohudhuria kuwa makini kwa kuwa ugonjwa huu ni hatari sana na unaua watu wengi kwa muda mfupi, hivyo tahadhari inatakiwa kuchukuliwa mapema.
Mganga Mkuu wa Wilaya Dr. Archard Rwezahula aliyesimama akitoa Mafunzo ya CORONA kwa Wadau Mbalimbali Katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya
Akianza kutoa Mafunzo Dr. Rwezahula amesema kuwa Ugonjwa CORONA -2019 ni ugonjwa wa kuambikiza unaosababishwa na kirusi kiitwacho Corona-2019 (COVID-19). Ugonjwa huu huathiri mfumo wa njia ya hewa (Pua, Koo na Mapafu). Aidha ameongeza Kuwa Mgonjwa wa kwanza alithibitishwa tarehe 31/12/2019 katika Mji wa Wuhan Nchini China, na ulitangazwa kuwa janga la Kimataifa na Shirika la Afya Duniani (WHO) tarehe 30/01/2020. Pia kwa Tanzania Mpaka sasa ni Mgonjwa Mmoja amethibitika kuwa na Corona na alitokea nchi za Denmark na Ubeligi.
Njia mbili za Kuambukiza Ugonjwa wa Corona-19
1. Unaambikizwa kwa njia ya hewa iliyochafuliwa na virusi vya Corona-19 kutoka kwa binadamu kwenda binadamu.
2. Unaambikizwa kwa kugusa vitu vilivyochafuliwa na virusi vya corona kama vile vitasa, meza na simu na kisha kujigusa mdomo, pua au macho.
Dalili za Ugonjwa wa Corona-19
1. Kikohozi, 2. Mafua makali na Chafya za mara kwa mara, 3. Kupata maumivu ya kichwa 4. homa, 5. kupumua kwa shida 6. Mwili kuchoka , 7.Vidonda kooni, 8. Maumivu ya misuli.
Namna ya Kujikinga na Kuwakinga Wengine.
1. Kunawa mikono mara kwa mara kwa maji yanayotiririka na sabuni au kutumia kitambaa chenye "alcohol based hand rub" kama vile:- baada ya kukohoa au kupiga chafya, baada ya kumhudumia mgonjwa, kabla,wakatika na baada ya kuandaa chakula, kabla ya kula, baada ya kutoka chooni, ukiona mikono yako ni michafu na baada ya kushika wanyama au uchafu wa wanyama.
2.Kutunza usafi wa njia ya hewa kwa kufuika mdomo na pua wakati wa kukohoa au kupenga makamasi kwa kutumia karatasi laini/kitambaa/kiwiko cha mkono. Kisha tupa karatasi laini uliyotumia sehemu (pipa) iliyofunikwa au kwenye shimo la taka.
3. Kaa umbali wa mita 1 (futi 3) kutoka kwa mtu anayekohoa au kupenga makamasi, na epuka kugusana, kushikana mikono na kubusiana.
4. Epuka kujishikashika macho, pua na midomo.
5. Jitahidi kupata taarifa sahihi na mpya za mlipuko wa ugonjwa wa Corona-2019.
6. Ukiwa na dalili zilizotajwa hapo juu fanya yafuatay:-tafuta tiba haraka, kaa nyumbani, usichanganyike kwenye makundi ya watu na toa taarifa kwa wataalam wa afya.
Chanjo na Tiba
Ugonjwa wa Corona -19 hadi sasa hauna chanjo wala tiba, ila mgonjwa hutibiwa dalili tu kama vile homa anapewa dawa ya kushusha homa, maumivu ya kichwa anapewa dawa ya kupunguza kichwa kuuma, mafua anapewa dawa ya kupunguza mafua makali, kuongezewa maji, kushindwa kupumua anawekewa vifaa vya kusajia kupumua na hewa ya oksijeni.
Athari za Ugonjwa wa Corona-19
1. Kiafya: Watu kudhoofu, idadi ya wagonjwa kuongezeka katika vituo vya kutolea huduma ya afya kuliko uwezo wa watoa huduma kuhudumia, na vifo
2. Kiuchumi: Kushuka kwa kiwango cha uzalishaji mali, gharamaza matibabu kupanda, na biashara zimesimama.
3. Kijamii: Kusitishwa kwa shughuli za kijamii kama vile michezoo na tafrija, shule zimefungwa, shughuli za idada zimesimamishwa, safari zimesitishwa na hofu kwa watu na jamii nzima.
Wadau Mbalimbali wakisikiliza Mafunzo ya Sahihi ya Corona-19 katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya
Baada ya Mfunzo haya kwa wadau, Mkuu wa Wilaya Ametoa maagizo yafuatayo ili yakatekelezwa na kila mdau na ameahidi kukagua utekelezaji wake na apate namna maagizo yalivyotekelezwa kwa maandishi. Maagizo hayo ni kama yafuatayo:-
1. Kuthibiti hofu kwa wananchi ila tuma kilasababu ya kuchukua tahadhari
2. Tuepuke mikusanyiko isiyo ya lazima mfano sherehe, naomba msogeze mbele mpaka hapo hali itakapokuwa salama.
3. Kuepuka safar zisizo na ulazima mfano Kusafiri kutoka mkoa moja kwenda mwingine bila sababu ya msingi.
4. Watu wa idara ya Afya waliopewa mafunzo ya Corona-19 waende katika taasisi zote na maeneo yote ili kutoa elimu kwa wananchi kabla ya Alhamisi ya tarehe 19/03/2020.
5. Kutenga maeneo ya kuwaweka watu watakaobainika kuwa wameambukizwa ugonjwa wa Corona-19.
6. Tuepuke kuwanyanyapaa wagonjwa hao kama watabainika ila unatakiwa kutoa taarifa.
7. Hakuna mtu yeyote kutoa taarifa ya mgonjwa bila kuwapata taarifa hiyo tka malaka husika kama unaona hisi kuna mtu anadalili hizo toa taarifa.
8. Kila taasisi iweke maji yanayotiririka na sabuni pamoja na sanitizers.
9. Kuwabaini wageni wote wanaotoka nje ya Nchi na hata nje ya Mkoa.
*********Mwisho*********
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.