Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amelazimika kuitisha kikao cha dharura na wamiliki wa nyumba za kulala wageni (guest, lodge and hotel) baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa utoaji huduma wa nyumba hizo za wageni wilayani Mpwapwa. Kikao hicho kimewahusisha, wamiliki wa nyumba za kulala wageni, maafisa mazingira, afisa biashara, maafisa tarafa na baadhi ya watendaji wa kata. Vilevile makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Mpwapwa wamehudhuria katika kikao hicho.
Wajumbe wa kikao cha wamiliki wa nyumba za kulala wakifuatilia maagizo na maelekezo ya mkuu wa wilaya ya Mpwapwa (Picha na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mhe. Shekimweri katika hotuma yake ya ufunguzi wa kikao hicho amesema kuwa kwa taarifa alizonazo kuna baadhi ya wamiliki wa nyumba za kulala wageni wanaendeleza kujenga guest zingine kiholela bila kufuata taratibu, wengine wanahifadhi machangudoa, kukaribisha watoto chini ya umri wa miaka 18 kama wateja wao, kutoa huduma ya chapu chapu (short time) na kuruhusu vibaka kuwaibia wateja. Aidha ameongeza kuwa baadhi ya nyumba za kulala wageni hazi zingatii kanunu za usafi wa mazingira hasa usafi wa choo, chumba, mashuka na mazingira ya nje. Pia ameonya hatasita kumchukulia hatua mmilikia atakaebainika anaenda kinyume na kanunu za umiliki wa nyumba hizo.
Mmoja wa wamiliki wa nyumba za kulala wageni akidai kuwa wahudumu wao ndio wanaowahujumu hivyo kuanzia leo watawasimamia wahudumu na hakutakuwa tena na huduma za chapuchapu na mambo mengine yasiofaa. (Picha na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Akitolea mfano Mhe. Shekimweri kuwa nyumba za kulala wageni za Zanzibar hawaruhusu wateja kulala katika chumba kimoja kama jinsia zao ni sawa, pia kama mwanamke na mwanaume wasio na vyeti vya ndoa na watoto wadogo waliochini ya umri wa miaka 18 bila mzazi wa jinsia sawa na ya mtoto huyo. Hii imepunguza sana hali ya vitendo vialifu na unyanyasaji wa kingono kwa watoto. Hivyo ametoa wito kwa wanamiliki wa nyumba za kulala wageni wilayani Mpwapwa waige mbinu hizo.
Vilevile Mkuu wa Wilaya huyo amewataka wamiliki hao kutokutumia vitabu viwili mpaka vitatu kwa lengo la kutoa takwimu za uongo kwa maafisa mapato na kupoteza mapato, ikibainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhini yao.
Mwisho, sambamba na maagizo hayo Mkuu wa Wilaya amewakumbusha wamiliki hao wa nymba za kulala wageni kuwa kuna ujio wa reli ya treni ya mwendo kasi (Standard Gauge) yenye fursa kemkem itakuwa na kituo wilayani Mpwapwa kata ya Gulwe, hivyo wawekeza sana katika nyumba bora, nzuri na za kisasa za kulala wageni, vyakula na biashara mbalimbali kwa kuwa tunatarajia kuwa na wageni wengi sana kutoka nje na ndani ya nchi ya Tanzania kufika Mpwapwa.
Mmoja wa wamiliki wa nyumba za kulala wageni akidai kuwa hakuwa anajua kuwa reli ya mwendokasi itakuwa na kituo mpwapwa na hivyo amemshukuru Mkuu wa Wilaya Mhe. Jabir Shekimweri kwa kuwafafanulia fursa zitakazopatikana baada ya reli kukamilika. (Picha na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.