Na: Shaibu J. Masasi; Afisa TEHAMA - Mpwapwa Dc.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amepokea msaada wa Ndoo chirizi 25 toka kwa Walimu wa Shule za Sekondari na Msingi waliopo Wilaya ya Mpwapwa katika kusaidia Mapambano dhini ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Walimu hao pia na wanachama wa Chama Chama Mapinduzi walioguswa na kuamua kuchangia juhudi za Serikali ya Awamu ya tano katika kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19.
Mhe. Shekimweri amesema "Nawapongeza sana ninyi walimu kwa kutoa sehemu ya mishahara yenu na kuamua kujitolea kuchangia mapambano dhini ya virusi vya corona. Hii ina maanisha kuwa mmeguswa na athari za ugonjwa wa covid 19 ambapo umesababisha taasisi za elimu kufungwa nanyi ndio wadau wa elimu, hivyo inaonyesha mnahitaji janga hili liishe ili mrudi katika majukumu yenu kama kawaida".
Mkuu wa Wilaya ameongeza kuwa " kupitia ninyi naomba wadau wengine waamasike katika kuchangia mapambano dhini ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona"
Pia amesema kuwa ndoo chirizi hizo zitagawanywa katika maeneo muhimu kama minadani, sokoni na kituo cha mabasi ili kuwakinga watu wanaopata huduma katika maeneo yenye mikusanyiko.
Mwisho amewashukuru wananchi wa wilaya ya Mpwapwa kwa kuitikia wito na maagizo ya serikali ya kuweka ndoo chirizi zenye maji safi na sabuni kwa kila nyumba, taasisi za umma na binafsi ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona na hivyo kupunguza maambukizi.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.