Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi H Ally amefungua Kongamano la Walimu Spesho lililoandaliwa na Bank ya NMB leo Julai 19 2025 katika Ukumbi wa CCM Mpwapwa.
Lengo la kongamano hilo kwa walimu ni kupewa fursa ya kutoa maoni na mapendekezo juu ya huduma zinazotolewa na Bank ya NMB.
Pia kwa upande mikopo Bank ya NMB wamepewa pongezi kwa kutoa mikopo kwa wingi kwa watumishi wa Serikali kuu na Serikali za Mitaa,pia kujali mahitaji ya wafanyakazi.
Halikadhalika ametoa raia kwa walimu hao kutumia fursa waliyopatiwa vizuri kwa kujifunza masuala ya kibank ikiwemo mikopo,bima,amana na huduma mbali mbali za NMB ambazo zitawasaidia si kiuchumi hata kuweka hakiba ya baadae ili kuweza kukidhi mahitaji ya dhararu.
"Niendelee kuwapongeza NMB kwani mikopo hii imekuwa msaada sana kwa wafanyakazi katika kukidhi mahitaji mbali mbali katika ngazi za familia na hata kufanikisha maandalizi yao ya baadae pale watakapo staafu"
"Natoa rai kwenu kutumia fursa hii vizuri kujifunza masuala ya kibanki ikiwemo mikopo,bima,amana,na huduma mbali mbali ambazo zitawasiadia sio tu kiuchumi bali pia kujenga utamaduni wa kuweka hakiba."Amesema Mkurugenzi Mtendaji
Nae Meneja mahusiano kutoka Makao makuu Bi Rita Majahasi ametoa mafunzo kuhusu utumiaji wa mfumo wa Utendaji wa Kiutumishi (ess) na utunzaji wa nywila kwa kila mtu huku akiwasisitiza kina mama zaidi kuwa makini n utunzaji wa nywila kwani kesi nyingi zinazotokea zinawahusu wao.
Hata hivyo ameainisha aina mbali mbali za mikopo zinazopatikana katik Bank hiyo ikiweko,Ada ya Elimu,ukarabati wa nyumba,kujengewa nyumba,kilimo kununuliwa nyumba kwa riba ya13% kuazia mwaka 1_5 na kuanzia miaka 6 _14 kwa riba ya 16%
Halikadhalika amebainisha njia mbili za ulipaji wa mkopo wa nyumba ikiwemo kupitia mshahara wa mkopaji au kulipa kupitia biashara yake binafsi.
Vilevile ameelezea elimu ya fedha inahusiana na matumizi ya kifedha ambayo itamsaidia mtumiaji mahsusi kwa malengo maalum na kutambua matumizi ya lazima kama vile chakula,mavazi,malazi na matibabu,ada na bili na matumizi yasiyo ya wazima.
Kongamano hilo lilishindikizwa na maandamano yaliyoanzia Tawi la Bank la NMB hadi Ukumbi wa CCM Mpwapwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.