Nendeni mkawasimamie watoto wetu wanaotarajia kufanya mtihan wa darasa la pili.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 15,2025 katika Ukumbi wa Chuo cha Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi H.Ally alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Walimu wa Msingi kutoka Shule Mbali mbali za Mpwapwa.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji amesema huu ni mpango wa mwanzo wa kufanya mtihani wa Taifa wa darasa la pili,ni matumaini yangu kwamba sote tutaweza kufuatilia kwa makini na kupata mbinu mbalimbali ambazo zitatumika katika kuwatahini wanafunzi wetu.
"Ni jambo jipya ambalo tunapaswa kulielewa ndio maana tuna wakufunzi hapa ambao wamekwenda kupikwa kwa siku sita,wamepata mafunzo haya na leo wanayafikisha kwenu,ni matumaini yangu kwamba sisi wote tutaeeza kufuatilia kwa makini"Amesema Mkurugenzi"
Kwa upandea wake Mwalim Mbate Almasi ameeleza kuwa,mafunzo waliyopatiwa ni yauboreshaji wa kada ya elimu kwa darasa la awali,la kwanza pamoja na la pili.
Lengo kuu la mafunzo hayo ni kutambua matumizi ya kiunzi cha upimaji cha Kitaifa,ikiwa na maana ya muongozo wa namna gani yakuweza kuwatahini wanafunzi wa darasa la la pili katika mahiri zao tatu ambazo ni Kusoma Kuandika na Kuhesabu.
Vilevile ameelezea matumizi ya zana ambazo zinatumika kwa mwalim katika upimaji wake,kama vile muongozo wa Kitaifa wa upimaji wa Standi za Kkk darasa la pili,saa na vielenzo.
Hata hivyo,wameweza kujifunza miongozo ya kusahihisha stadi zote tatu na namna ya kupakua na kupakia vielenzo pamoja na mitihani kutoka kwenye mfumo,pia namna ya kutahini kwa wanafunzi wa kawaida na wenye mahitaji maalum
Nae, Mkurugenzi Mtendaji amewapongeza Walimu wote wa Msingi pamoja na viongozi wake kaa ujumla kwa matokeo mazuri ya Darasa la saba na darasa la nne.









Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.