Wakulima wa Wilaya ya Mpwapwa wanufaika na mkopo wa vitendea kazi kwa mwaka wa tatu,na jumla ya Powertila 27 zimetolewa, na ikiwa leo Septemba 27,2024 wapatiwa nyengine 10 kutoka kwa wadau wa Bank ya Equit ikiwa ni utaratibu wa kila mwaka kuwapatia wakulima mkopo huo.
Mbali na mkopo wa vitendea kazi pia hutoa mkopo wa maandalizi ya shamba na kupalilia
Mkuu wa Idara ya kilimo Bi Maria Lishalo amesema wakulima ambao wanaopatiwa powertila hizo huzitendea haki kwa kuzitumia ipasavyo na kurejesha marejesho ya mkopo kwa wakati sababu inayopelekea mtoa mkopo kuendelea kutoa mkopo huo kwa kila mwaka.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri amesema powertila hizo zitasaidia kuleta maendeleo binafsi na Wananchi kwa Ujumla,pia amewashukuru wadau wa Bank ya Equit kwa kuendelea kutoa mkopo wa vitendea kazi kwa miaka mitatu bila ya kuchoka.
Pia,amewapongezawale waote waliopewa mkopo mwanzo na kurejesha kitendo ambacho kimejenga dhamana kubwa iliyopelekea na wengine kukopeshwa.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.