Viongozi wa Vijiji na Maafisa ugani wa Gulwe,Mzase na Msagali wamepata mafunzo ya mradi wa BASIN
yanayohusiana na taarifa za tahadhari ya mapema ili kuweza kukabiliana na majanga ya hali ya hewa kutokana na mabadiliko ya tabianchi Septemba 11,2025 katika Ukumbi wa Tumaini
Mkurugenzi kutoka Shahidi wa Maji ameieleza BASIN ni kuwa mradi wa kiutafiti unaojaribu kuunganisha,kutathmini,na kutumia maarifa kutoka katika Sayansi ya tabia na saikoloji ili kuimarisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuengeza uhakika wa maji uliojumuishi kwa makundi yaliyo hatarini zaid.
lengo la mradi ni kutoa tahadhari za mapema na kutoa taarifa ya hali ya hewa kuweza kutumika sawa sawa kwa wakulima na wafugaji ili waweze kujiandaa na hali ya hewa ya baaadae,hii ni kutokana na matokeo ya tafiti zilizofanyika na kubainika taarifa za hali ya hewa hazifiki kwa wananchi na wala hakuna taarifa mahsusi inayotolewa kutoa tahadhari.
Taarifa ya matarajio ya hali mbaya ya Hali ya hewa kwa Mpwapwa imewasilishwa ikiambatana na angalizo,uwezekano wa kutokea kwa majanga pamoja na kiwango cha athari zinazoweza kutokea.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.