Na: Shaibu J. Masasi; Afisa TEHAMA - Mpwapwa Dc
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Mussa Shekimweri amekutana na viongozi wote wa tarafa ya Mpwapwa ili kuwapatia Mikakati ya Wilaya ya kupambana na Ugonjwa Hatari wa Corona (COVID-19) unaosambaa kwa kasi katika Nchi nyingi duniani, ambapo kwa sasa Nchi ya Tanzania imethibika kuwa na wagonjwa 12.
Katika Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya Umehudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usala ya Wilaya, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mpwapwa Mjini, Ndugu. Paul M. Sweya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Wataalam toka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Katibu Tarafa ya Mpwapwa, Watendaji wa Kata wote, Wenyeviti wa vijiji na Wenyeviti wa Vitongoji.
Aidha viongozi hao wamepatiwa elimu sahihi ya corona kuanzia maana ya ugonjwa wa Corona-19, unavyosambaa au kuambukizwa, dalili zake, jinsi ya kujikinga na namna ya kupata msaada ya matibabu iliyotolewa na Daktari Kikoti Jumaa Morijo toka Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa. Pia viongozi waliohudhuria Kikao hicho wamepewa vipeperushi vilivyotengenezwa na Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Msalama Mwekundu (RED CROSS) ili kuwawezesha wananchi kufahamu mambo ya msingi katika kujilinda na ugonjwa huu wa corona. Katika vipeperushi hivyo kumeelezwa maana ya corona-19, jinsi ungonjwa unavyoosambaa, dalili za corona, jinsi ya kijilinda na jinsi ya kupata msaada wa matibabu.
Kipeperushi Kuhusu Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu Unaosababishwa na Virusi vya CoronaDaktari Kikoti wa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa ambaye pia ni Moja kati ya Waelimishaji toka katika Timu ya Wilaya ya Waelimushaji Juu ya Corona
Katika kikao hicho viongozi wa tarafa ya Mpwapwa wameelimishwa juu wa Ugonjwa wa COVID-19 na kupewa fursa ya kuuliza maswali na maswali yote yamejibiwa vizuri na hivyo kuimarisha uelewa wa washiriki hao. Pia viongozi hao wameahidi kwa kushirikiana na wataalam wa Afya na wajumbe wa Timu ya Wilaya ya Udhibiti dhidi Corona kwenda kutoa elimu hii kwa wananchi wanaowaongoza.
Baada ya Viongozi hao kujengewa uelewa juu ya Ungonjwa wa Corona, Mkuu wa Wilaya Mhe. Shekimweri alipokeza usikivu mzuri uliofanywa na viongozi hao waliohudhuria kikao hicho na kuuliza masawali ya msingi yenye kutaka kuelewa vizuri ugonjwa huu. Pia amempongeza Daktari Kikoti kwa kusema "Daktari umetoa mafunzo mazuri kwa kutumia lugha nyepese ya kiswahili ambapo kila mmoja ameelewa".
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka viongozi na wananchi kuondoa hofu ila kuchukua tahadhari dhidi ya corona, kufanya kazi kwa bidii, kuepuka mikusanyiko isiyo yalazima, kuacha safari zisizo za lazima na kukaa umbali wa mita moja toka mtu mmoja hadi mwingine kila tunapokaa na kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni mara kwa mara.
Mkuu wa Wilaya amesema kwamba "Wilaya ya Mpwapwa imejipanga kikamilifu katika kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa corona kwa kuunda kamati 5 za kuelimisha juu ya corona, kuweka mikakati ya Kila taasisi kuweka ndoo ya maji yanayotiririka na sabuni na kufanya vikao na watumishi. Pia ameongeza kuwa "Wilaya imetenga Logde ya Chichi, Ark hotel na Kalunguyeye zitapokea washukiwa wa ugonjwa wa corona-19 waliosafiri toka nje ya nchi na watajigharimia wenyewe kwa siku 14".
Vilevile Mkuu wa Wilaya amesema kuwa "Kama kukitokea wagonjwa wa corona katika Wilaya yetu, kila zahanati na vituo vya afya vimetengwa vyumba kwa ajili ya kuwapokea wagonjwa wanaohisiwa kuwa na corona na kupatiwa matibabu ya dalili watakaoonyesha wakati majibu ya vipimo yanasubiriwa, tumetenga maeneo ya kuwahifadhi washukiwa wa ugonjwa wa corona kama watabainika katika wilaya yetu katika Chuo cha Ualimu Mpwapwa, Chuo cha Mifugo ( LITA), Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI), na zahanati ya Mazae kwa ajili ya kulazwa wagonjwa wa corona ".
Mwisho Mkuu wa Wilaya amewashukuru viongozi kwa kukubali wito wake na kutapa mafunzo ya corona na hivyo anatumaini watakuwa mabalozi wazuri kwa wananchi.
******Mwisho****
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.