Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe Dkt Sophia Mfaume Kizigo amefanya kikao maalum na Viongozi wa dini, Wazee maarufu na Machifu, kwa lengo la kujadili Elimu ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na namna ya Udhibiti wa Mmomonyoko wa Maadili kwa watoto na vijana.
Kwa upande wa elimu ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Afisa Uchaguzi Ndg;Thomasi Magali amehamasisha viongozi hao kwenda kutoa elimu kwa Wananchi wao kuchagua viongozi walio bora ili waweze kwenda sawa na kasi ya Mama Samia katika kuleta maendeleo ya Nchi.
Pia amesisitiza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ifikapo Octoba 11-20,lakini kawakumbushe kuchukua fomu za kugombea Uongozi kuanzia Novemba 1-7,ambapo Novemba 20-26 kampeni za wagombea zitafanyika na kusisitiza ziwe za amani na utulivu ili kuweza kupiga kura Kwa Usalama ifikapo 27 Novemba 2024.
"Kawasisitizeni wachague viongozi waliobora ili waweze kuendana na kasi ya Mama Samia,
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.