Viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Zanzibar wakiongozwa na Naibu katibu Mkuu Ndg Salhina Mwita Ameir wamefanya ziara ya kikazi Mkoani Dodoma wilayani Mpwapwa Mei 2,2025 kwa lengo la kujifunza kwa namna gani matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo zinavyotumika na Kuimarisha Muungano wa Tanzania.
Ndg Ameir amesema lengo kuu la ziara hiyo ni kuja kujifunza namna ya utekelezaji na uratibu wa fedha za mfuko wa kuchochea maendeleo ya Jimbo katika Halmshauri ya Wilaya ya Mpwapwa na kujengewa uwezo wa uelewa wa utekelezaji na usimamizi wa fedha za mfuko wa maendeleo Visiwani Zanzibar
Wakati wa ziara yao hiyo wametembelea vituo vya Afya Makutupa na Mlembule na kujifunza mambo mbali mbali ambayo yameweza kuwajengea uwezo mpya wajumbe yakiwemo kuwepo kwa Kamati Madhubuti za Ujenzi na mgawanyo wa majukumu kwa kila mwana kamati.
Pia wamepongeza kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo pamoja na kutumia vizuri hela za mfuko wa Jimbo ambazo wanapatiwa majimboni mwao kutoka kwa Wabunge wao.
Akihitimisha ziara hiyo Ndg Ameir ametoa shukrani zake za dhati kwa Ofisi ya Mkurugenzi na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa kwa mapokezi mazuri waliyo yaandaa na kujipanga katika ziara hiyo na kuridhika na miradi waliyoiona inaendana na mahitaji ya jamii husika na kuwasisitiza Wananchi waliopata miradi hiyo kuitunza na kuithamini.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.