Shirika la Umoja wa Mataifa la Utunzaji Mitaji na Uwekezaji(UNCDF)United Nations Capital Dèvelopment Fund limetambulisha mradi wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa awamu ya pili leo Januari 16,2025.
Awali Mradi huu ulifanyika mwaka 2017 kwa njia ya maandiko na ulipofika 2018 uliweza kutekelezwa kwa mipango mbali mbali na njia ya majaribio.
Lengo kubwa la Mradi ni kuijengea uwezo Nchi kupitia Halmashauri zake kutambua Mabadiliko ya Tabia Nchi na kutengeneza mipango ya kuhamasisha matumizi ya Rasilimali.
Pia kutengeneza mfumo wa kutoa fedha kwa ajili ya Halmashauri kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi,mfumo ambao huendeshwa kwa kukidhi vigezo na masharti na baada hapo hutumika,kama vile awamu ya mwanzo uliweza kutumika kwa kujenga kisima cha Kisisi wilayani Mpwapwa.
"Lengo letu kubwa ni tunajengea uwezo Nchi kupitia Halmashauri wa kutambua Mabadiliko ya Tabia Nchi na kutengeneza mipango ya kutambua rasilimali za nje na ndani"
"Mfumo unaangalia vigezo na masharti,vigezo vyake ni vipi na masharti yake ni yepi Mmeweza kuvikidhi na kuweza kufanikiwa?"amesema Dr Aine Mushi
Halikadhalika lengo la mwisho la mradi huu ni kujenga uwezo Halmashauri ili kuweza kutambua Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na kuweza kuyatambulisha ili kuyaingiza katika mipango na fedha nankuyatolea taarifa.
Kikao cha Wadau kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Utunzaji wa Mitaji na Uwekezaji(UNCDF)kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mpwapwa na kuhudhuriwa na Wakuu wa Idara na Viengo.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.